12/01/2023
BONGO MOVIE WAMEISHIWA!!
Habari zenu wadau wa Page hii?
Leo naomba kujadiliana nanyi kwenye maisha ya Bongo movies.
Ivi ni kwanini tumeshindwa kabisa kufanya filamu zetu kuwa vizuri ndani na nje ya Nchi zetu?
(1)Maoni yangu mimi tunashindwa kufanya vitu vizuri kwasababu hatupo Serious na vitu tunavyovifanya hii inatokana na kwasababu hatuna chombo/taasisi maalumu kinachosimamia mambo muhimu yanayotakiwa kuonekana kwenye hizi movie hivyo kila mmoja anajivyatulia tu filamu ili mradi aonekane kwenye Tv bila ya kujua kuwa anauwa soko la filamu nchini kwasababu filamu kumi zinazotoka mtu ameangalia 8 zote utopolo kesho na keahokutwa hawezi kuziangalia zile filamu mbili ambazo hajaziona,hiyo ni kwasababu tayari ameshatokwa na hamu ya bongo movies kupitia filamu 8 mbovu alizoangalia.
(2)Kutokuwa na misingi mizuri ya kazi tunazozifanya. Tunatumia kipaji zaidi kuliko elimu ya Darasani. Unapokuwa na kipaji ni vyema ukaongeza kitu ambacho kitaenda sawa na kipaji chako. Mfano mcheza mpira,wapo wengi wenye vipaji ila mazoezi na kusomeshwa mbindu za uwanjani k**a mambo ya kumkaba mchezaji wa timu pinzani ndio kunakufanya uwe bora zaidi kwenye soka
(3)Bajeti ya filamu. Wengi sana hatufanyi kitu kilichobora kwasababu ya bajeti yetu ni ndogo sana na hata baadhi ya cast huwa tunawachukuwa pasipo na malipo ya aina yoyote yale isipokuwa mein character tu ndio anaelipwa
(4)Story zetu ni mbovu na zenye kufanana fanana fanana na nyepesi sana kiasi cha kwamba mtu anaweza kuotea tukio litakalotokea mbele kiuhakika kabisa. Mfano msichana mzuri anaweza kumgonga muuza machungwa na mtu akaotea kuwa baada ya kumpeleka hospitali atampenda na ukakuta ndio hivyo hivyo 😜
(5)Hatupangilii step zetu za kuonyesha filamu husika. Tumekuwa tukifanya step moja tu ambayo ni kufyatua Cid na kuuza,wakati kuna step 1,2,3............
Mfano: kuonyesha Treilar la movie husika ili kuwaamsha watu kwa vionjo vya filamu yako,kuipeleka kwenye majumba ya Cinema,kuipeleka kwenye ma-Tv makubwa makubwa na mwisho wa siku kuivyatua kwenye CID Ili waone jumla jamala.
K**a una maoni zaidi tupia kwenye Comment hapo ili tuiyamshe Bongo movie yetu iliyolala usingizi mzito.
Karibu sana
My No. 0676004670