Huda Gharib

Huda Gharib Digital Content Creator
Teacher and Trainer

WHAT I'M AFRAID OF BEFORE I DIE ( Kinachoniogofya kabla ya kifo changu)Ninapofikiri kuhusu maisha yangu na safari iliyo ...
07/10/2024

WHAT I'M AFRAID OF BEFORE I DIE ( Kinachoniogofya kabla ya kifo changu)

Ninapofikiri kuhusu maisha yangu na safari iliyo mbele yangu, mara nyingi kuna hofu hunijia, hofu ya kupoteza maono ya lengo kuu la maisha na zawadi hii ya uhai na uzima. Katika zama hizi tulizonazo ni rahisi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta mali, mafanikio, na uthibitisho (sifa na vyeo vitokanavyo na hayo). Kila siku, tunakimbilia katika kujikusanyia vitu,tukipima thamani yetu kwa kujifananisha na wengine na kujitahidi kupanda ngazi isiyo na mwisho ya mafanikio. Hata hivyo, katika mbio hizi, nina wasi wasi kuhusu jambo moja..

Si jengine ila lile linalo nipa hofu kubwa kila wakati nalo ni kufika mwisho wa uhai wangu nikiwa na majuto na huzuni.Nadhani mara nyingi, tunatumia muda wa kutosha kwa mambo yetu binafsi ikiwemo ukuaji wa kibinafsi, na kutafuta maarifa. Lakini je ni kwa kiasi gani haya mambo yetu binafsi hutueka mbali na wengine ? familia na marafiki?

Je, tumetoa muda wa kutosha kweli kutambua uzuri wa ulimwengu na mazingira yanayonizunguka?

Zaidi ya hayo, ninahisi hofu wakati ninapowaza kuhusu ukomo wa uhai wangu . Wazo (idea) la kusimama mbele ya ukweli wa mwisho wa maisha yangu , nikitafakari jinsi nilivyotumia siku zangu.Je, niliishi kwa upendo? Je, nini kiliku kipaombele changu?

Kadri ninavyotafakari kuhusu umauti, nazidi kubaini ya kwamba kila sekunde hapa ulimwenguni ni zawadi. Masaa yanakatika, na kila kila kipimo cha muda ni muhimu.

Ila nimebaini hofu yangu si kifo chenyewe, bali wazo la kufa bila kuishi na kufikia lengo la kua ulimwenguni .Ewe nafsi yangu na ya mwenzangu kumbuka lengo kuu la Uhai wako hapa duniani, acha kupumbazika kwingi kwa kisingizio cha kutafuta mali na kukimbizana na kivuli cha mafanikio ya kidunia (yenye udanganyifu).

UNLOCKING THE  POTENTIAL WITHIN,THE METAPHOR OF PLANTING SEEDS AND BITTER FRUITS Ni miaka  kadhaa sasa tangu nilipo kwaa...
20/10/2023

UNLOCKING THE POTENTIAL WITHIN,THE METAPHOR OF PLANTING SEEDS AND BITTER FRUITS

Ni miaka kadhaa sasa tangu nilipo kwaana na nukuu hii katika mitandao ya kijamii, kiukweli hii ni moja ya nukuu niliyo ishare sana kwa muda sasa acha leo ni share nawe sura tofauti tofauti juu ya uelewa wangu na natumai utanufaika.

"Burry yourself in a barren, deep earth because a seed that is not planted won't ripen and at the least, it's fruits will be bitter"

Sura ya kwanza: Nguvu ya kuotesha mbegu za mafanikio

Mara nyingine tunaweza kuwa na wazo zuri la biashara lakini usiliteleze na lika baki story tu. Katika hali hii, wewe ni k**a mbegu ambayo haikupandwa. Bila vitendo, wazo lako linabaki kuwa hewa na lisilo maaana kwasababu utekelezaji ndio utakao zaa matunda ya wazo hilo. Kwa mfano, fikiria ... kampuni ngapi kubwa, k**a vile Apple na Google, zilianza k**a mbegu ya wazo, lakini zililazimika kupandwa kupitia kazi kubwa, kujitolea na kutumia muda mwengi bila uoga.

Sura ya pili 2: Faida ya kujiendeleza ujuzi

Fikiria mfano wa mtu anayetaka kuwa mwanamichezo maarufu. Ikiwa hutatumia muda wake na jitihada kujifunza na kufanya mazoezi, hataweza kukomaa kiujuzi na kufikia malengo. Ni k**a vile mbegu ambayo haiku pandwa katika udongo wa wenye rutuba . Kwa upande mwingine, mwaanamasumbi maaarufu Muhammad Ali alitumia maisha yake kujifunza na kufanya mazoezi, akipanda mbegu za kipaji chake katika udongo mzuri wenye rutaba na kuvuna matunda matamu ya kazi yake.

Sura ya tatu 3: Kujenga mahusiano ili kupata maisha yenye furaha.

Kujenga uhusiano ulio mzuri ni eneo lingine linalohusiana na nukuu hii. Bila kupanda mbegu za urafiki, ujirani mwema na undugu (maana waswahili husema udugu si kufanana), maisha yako yanaweza kuwa ya upweke na uchungu (Mwenzangu wee mambo na watu). Kwa upande mwingine, watu wanaowekeza kikamilifu katika mahusiano yao hufurahia matunda ya uhusiano wa kina na kuwa wenye furaha.

Ki msingi, nukuu hii inatukumbusha kwamba uwezo na mawazo ni k**a mbegu, inahitaji kupandwa na kulelewa kwa jitihada na uaminifu. Bila hivyo, hutaweza kufaidika na matunda (faida) yake. Kwa hivyo, ikiwa unayo ndoto, mawazo, au matarajio, usiyadharau na kuyaacha yapotea tu k**a vile na upepo bali pitisha jitihada yako ya kuyaandeleza maazimio yaliyo ndani yako.

SECOND CHANCE IN LIFE START WITH YOU!Nafasi ya Pili Maishani: Inaanza na WeweMaisha ni safari iliyojaa changamoto, vikwa...
18/10/2023

SECOND CHANCE IN LIFE START WITH YOU!

Nafasi ya Pili Maishani: Inaanza na Wewe

Maisha ni safari iliyojaa changamoto, vikwazo, na mizungukotofauyi tofauti. Mara nyingine, tunajikuta tukikabiliana na matatizo, vikwazo, na vipindi vya huzuni na kutufanya tutamani nafasi ya pili (second chance). Lakini ukweli ni kwamba nafasi ya pili inaanza na wewe. Unachotakiwa ni kuweza kujiamini, na kujenga ujasiri wa kuchukua udhibiti wa hadithi yako mwenyewe.Fanya haya kubadili hadithi yako ya maisha

1.Jisamehe
Moja ya hatua za kwanza katika kujipatia nafasi ya pili ni kujisamehe. Sote tunafanya makosa, kushindwa katika mambo mbakimbali, na kuishia kwenye maputo na kujilaumu. Lakini kushikilia mzigo huu wa lawama juu yako kunaweza kuzuia maendeleo. Jifunze kujisamehe, acha yaliyopita, na jipe nafasi kwa ajili ya ukuaji wako kibinafsi.

2. Tathmini upya malengo yako
Ili kuanza upya, tathmini malengo yako maishani. Unataka kufikia nini kwa kweli? Ndoto gani umeweka pembeni? Kamwe hujachelewa kurekebisha malengo yako na kufanya kazi kuelekea kuyafikia. Nafasi ya pili mara nyingine inamaanisha kufanikisha malengo yako na ndoto zako binafsi.

3. Jifunze kwa yaliyopita
Kupitia yote yaliokukwanza hapo nyuma kwenye maisha yako bila shaka utaweza kupata mafunzo mengi, Waswahili husema ukupigao ndio ukufunzao hivyo tafakari vizur juu ya Changamoto, vikwazo na makosa kwenye siku zilizopita na utumie kujenga mustakali mzuri wa maisha yako.

4. Jichanganye watu wenye mitazamo chanya juu ya maisha.
Waswahili husema kila mkaa na waridi hunukia lakini pia tibia zako za kila siku zinaathiwa mno na watu waokuzunguka , hivyo basi watu utakoshirikiana nao wanaweza kuathiri sana nafasi yako ya pili (secondchance). Amiliana na watu wanaokusaidia katika ukuaji wako, kuchochea ndoto zako, na kutoa nishati chanya (positive energy). Kujenga mtandao wa kusaidiana unaweza kuwa kipengele muhimu katika safari yako ya kujiboresha.

5. Chukua Hatua
Nafasi ya pili haitokei tu, unahitaji kuchukua hatua. Iwe ni kufuatilia kazi mpya, kurekebisha mahusiano, au kuanzisha tabia za afya k**a vile kufanya mazoezi ama mpangilio wa ulaji, inaanza na uamuzi wa kubadilika. Kuwa mwenye bidii na chukua hatua ndogo kuelekea malengo yako kila siku.

6. Jenga Uthabiti ( Consistency)
Changamoto za maisha zinaweza kutikisa uthabiti wako, lakini ni uwezo wako wa kusimama imara na kutambua safari yako. Jiandae kwa vikwazo, lakini kamwe usiruhusu vikwazo hivyo vikusimamishe kufikia mustakabali bora. Uthabiti (Consistency)ni mkuu msingi wa nafasi ya pili.

7. Jali Kujitunza
Mara nyingi tunapopitia vipindi vigumu maishani wengi hutolea maaanani suala la kujitunza. Kujitunza iwe kimwili na kiroho ( imani), ni muhimu. Tanguliza kujitunza mwenyewe ili kuweza kudumisha mtindo wa maisha wenye afya, kutafuta msaada unapohitajika, na kutunza ustawi wako wa akili. Kuanza upya mara nyingine kunahitaji mwili wenye afya na akili timamu.

8. Kuwa na subra
Roma hakuwa jengwa kwa siku moja, hivyo hivyo pia nafasi yako ya pili itachukua muda. Kuwa na subira binafsi lakini pia kwenye maendeleo yako. Kila hatua mbele ni ushindi, na nafasi ya pili ni mchakato, sio mabadiliko ya haraka.

9. Weka imani thabiti ( Amini)
Amini katika uwezo wako na uwezo wako wa kujenga mustakabali bora. Nafasi ya pili katika maisha inaanza na imani thabiti kwamba una nguvu na inshaAllah utashinda vikwazo na kujenga maisha unayotamani. Kumbuka, nguvu ya kuanza upya iko ndani yako.

Hakika!! Haijawahi kua rahisi
27/07/2023

Hakika!! Haijawahi kua rahisi

Angalia kinachoendelea viwanja vya Kariakoo
25/04/2023

Angalia kinachoendelea viwanja vya Kariakoo

Ni rahisi kuelemewa na yote yanayoendelea na kukengeushwa kutoka katika lengo lako kuu. Kwa kuwa ni kipindi cha Ramadhan...
02/04/2023

Ni rahisi kuelemewa na yote yanayoendelea na kukengeushwa kutoka katika lengo lako kuu. Kwa kuwa ni kipindi cha Ramadhani , endelea kujikumbusha yaliyo muhimu. Usitumie muda kwa shughuli zisizo na maana zinazokuweka mbali na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Endelea kuzingatia,kua na msimamo thabiti,mkarimu na mwenye kusamehe.
Kuwa na furaha sio tu kwako, bali kwa wengine pia. Kuwa na shukurani kwa neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu amekuletea. Kubali na jifunze kutokana na mitihani yoyote anayokuletea. Kuna masomo na baraka katika yote ikiwa unaweza ukatilia maanani kujifunza. Ramadhani hii, weka dhamira thabiti ya kutumia maneno kuwajenga watu. Acha kutumia lugha chafu, usemi mbaya na usilaani na kuapa, maneno yana nguvu sana, huaaacha athari ya kudumu. Kwa hiyo usiruhusu kitu kingine isipokuwa chema kitoke kinywani mwako.

Address

Zanzibar City

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Huda Gharib posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Huda Gharib:

Share