Tukuyuwssa

Tukuyuwssa Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tukuyuwssa, Camera/Photo, Bomani, Tukuyu.

Mamlaka ya maji Tukuyu inatoa huduma ya maji Safi na salama kwa wakazi wa mji wa Tukuyu kupita vyanzo vyake vya maji vilivyopo katika hifadhi ya Mlima Rungwe na Kibisi.

26/06/2026
Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Tukuyu mapema leo tarehe 27/03/2026 wametoa elimu ya huduma ya maji kwa Mabalo...
27/03/2026

Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Tukuyu mapema leo tarehe 27/03/2026 wametoa elimu ya huduma ya maji kwa Mabalozi wa mitaa ya eneo la Makandana kuhusiana na huduma ya Maunganisho ya maji, matumizi ya Dira za maji na namna ya utatuzi wa malalamiko ya Wateja.

Aidha, Mamlaka imeomba ushirikiano wa utatuzi wa changamoto ya mivujo kwa kuomba kupewa taarifa kwa kuwa pia imelalamikiwa na Viongozi hao na kuonekana upotevu mkubwa wa maji unatokana na mivujo. Mamlaka imeeleza kuwa imeunda timu itakayokuwa inashirikiana na viongozi hao katika kupita mtaa kwa mtaa kubaini na kuziba mivujo.
Maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wajumbe wa kikao yamechukuliwa na Maafisa wa Mamlaka ya Maji kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji Tukuyu Mjini hususan Makandana.

Waziri mkuu Mhe. Lamech Mwiguru Mchemba (mb) leo tarehe 24/2/2026 ikiwa siku ya pili ya Mkutano akiwa mgeni rasmi katika...
24/02/2026

Waziri mkuu Mhe. Lamech Mwiguru Mchemba (mb) leo tarehe 24/2/2026 ikiwa siku ya pili ya Mkutano akiwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za maji Nchini uliofanyika Jijini Arusha. Ameipongeza Sekta ya maji kwa kufikisha huduma ya maji maeneo mengi Tanzania sambamba na kuitaka Sekta hii ya maji pamoja na wananchi kwa ujumla kutunza vyanzo vya maji, kudhibiti mivujo ya maji, kufikisha huduma ya maji maeneo yaliyosalia pamoja na kudhibiti ubambikizaji wa Ankra za maji kwa Wateja.

‎Vilevile amesisitiza kila Mamlaka ya maji kuhakikisha Kila shule ya Msingi, Sekondari, vituo vya afya na Hospitali zipate huduma ya maji toshelevu

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Tukuyu wamehudhuria Mkutano wa Bodi za Wakurugenzi wa Mamlaka za M...
23/02/2026

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Tukuyu wamehudhuria Mkutano wa Bodi za Wakurugenzi wa Mamlaka za MajiSafi na Usafi wa Mazingira Mchini unaofanyika kuanzia tarehe 23/2/2026 hadi tarehe 25/2/2026 Jijini Arusha katika ukumbi wa Ngurdoto mgeni rasmi akiwa Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb).

Kauli mbiu:
"Maji Kwa wote: Kuimarisha Uhimilivu, Uendelevu wa Kifedha na
Utoaji wa Huduma Bora Nchini"

Address

Bomani
Tukuyu

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tukuyuwssa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category