Aden kisimbe

Aden kisimbe Life coach and video graphic

02/09/2022
28/07/2022

Kuna mambo Mungu anakuruhusu Uyapitie ili uje kuwa Msaada Kwa wengine.

Anakupa “Experience” muhimu ili uwe mwalimu mzuri kwa watu wengine hapo baadaye.

Masomo ya namna hii wakati mwingine yanaambatana na maumivu...
..kukataliwa na aibu ila ndio sehemu ya mtaala wa somo lako ili uandaliwe vizuri.

Sio kila unachopitia ni kwa ajili yako, kuna mengine yanakuandaa kuwa msaada kwa wengine.

Unapitia makosa ambayo ulidhani usingeweza kuyafanya...
..ili ukikutana na mtu aliyekosea USIMUHUKUMU.

Unapitia maumivu yanayodhihirisha udhaifu wako...
..ili ukikutana na na mtu aliyepatwa na aibu UMSITIRI.

Unakutana na kufeli katika kitu ulichokuwa na uhakika 100% kuwa utafaulu...
..ili ukikutana na aliyefeli usimuone mzembe bali UMTIE MOYO.

Unapitia hali ngumu ya maisha na kukosa pesa...
..ili siku mtu akihitaji msaada wako kidogo unakuwa unaelewa maumivu ya kushinda njaa na kutokuwa na pesa.

Unapitia kipindi unabaki peke yako na hakuna wa kukusaidia...
..ili siku ukikutana na mtu aliyeachwa na awapendao uelewe maumivu anayopitia na UMSAIDIE.

Kuna mambo ni k**a kusomea udaktari, unasoma mambo magumu kwa miaka mingi...
..ili uwasaidie wengine watakapougua. Kuna masomo ya maisha unayapitia leo ili uwe mwalimu na msaada kwa wengine.

Nakuombea, Mungu akupe nguvu usikimbie darasa bali UFAULU.

Je Unataka....

1. Ufikie Malengo Yako Ya Kifedha kwa kasi?

K**a jibu lako ni NDIO basi Video za kozi zangu zote 5 ndio mkombozi wako.

Na k**a BONUS nakupa eBooks zangu 2 MPYA ZAIDI.

1. Kipaji.

2. Vita Ya Mkombozi Wa Familia.

Thamani ya kozi hizi zote 5 na eBooks zangu 2 MPYA zaidi ni zaidi ya Tsh 200,000.00

Ila LEO utavipata hivi vyote kwa Tsh 10,000 Tu!

Kupata kozi hizi na BONUS zake SASA HIVI

Tuma Tsh 10,000 Tu!

Kwenda M-PESA

0762 312 117 (Joel Nanauka)

Kisha tuma UTHIBITISHO WA MUAMALA na neno "KOZI" kwenda

Whatsapp +255 762 312 117

24/07/2022

Mbinu Kuu za Kuweka Bei Sahihi Itakayofanya Uuze Zaidi.

____1. Bei Ya Kupenyea Kwenye Soko.

Bei hii hutumika k**a unataka kuingiza bidhaa mpya sokoni au kuingia kwenye soko ambalo haujawahi kuwepo kabisa.

Unaweza kuweka bei hii kwa njia zifuatazo:

a. Kutumia Break Even/Production Cost:

Hapa unauza bila faida na bila hasara. Unaweka bei sawasawa na ile ya gharama za kuzalishia bidhaa husika.

Hapa nia kubwa ni kufanya bidhaa yako ijulikane kwa haraka kwa kuwa rahisi kununuliwa sokoni.

b. Unaweka Faida Kidogo Sana:

Hapa unaweka bei zaidi ya gharama za uzalishaji, ila bei yako inakuwa ndogo sana ukilinganisha na watu wengine wanaouza bidhaa k**a za kwako sokoni.

Mara nyingi bei hii sio ya kudumu, unaanza nayo na kisha baada ya muda baada ya watu kutumia kwa muda fulani.

Tunaanza kuiongeza bei ya bidhaa/huduma taratibu taratibu hadi utafika bei ya kupata faida unayoitaka.

Faida ya kutumia mbinu hii ni kuwa utavutia watu wengi haraka sana pale ambapo unaanza kuitumia.

Hasara yake ni kuwa utakapoanza kuongeza bei, k**a utaongeza kwa haraka watu watakukimbia baadaye.

Falsafa ya kutumia bei hii ni kuwa badala ya kuweka gharama kubwa kwenye matangazo, unaamua ile faida ndogo unayopata/uliyoipoteza ndio inakuwa gharama yako ya matangazo kwa kuvutia wateja.

Kujifunza kwa kina zaidi nashauri usome eBooks zangu zinazohusu Biashara.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi.

2. Saikolojia Ya Mteja.

3. Hatua 6 Za Kujiajiri, Jinsi Ya Kujiingizia Kipato Kwa Kazi Yako Mwenyewe.

4. Mbinu Za Kuongeza Kipato Chako.

5. Money Formula, Elimu Ya Fedha Isiyofundishwa Shuleni.

6. Namna Ya Kuondokana Na Madeni.

7. Nifanye Biashara Gani?

8. Tabia 12 Zinazoleta Mafanikio.

9. Mafanikio Ya Kifedha Kwa Wanandoa.

10. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

Thamani ya eBooks hizi zote ni zaidi ya Tsh 50,000.00

Ila leo nitakupa eBooks hizi zote kwa Tsh 10,000 Tu! kupitia Whatsapp yako ukiwa popte duniani

Kuipata eBooks hizi SASA HIVI

Tuma Tsh 10,000 Tu!

Kwenda M-PESA

0742 112 946 (Joel Nanauka)

Kisha tuma uthibitisho wa muamala na neno "BIASHARA BANDO"

Kwenda Whatsapp 0742 112 946

Ndani ya masaa 24 utatumiwa eBook yako kupitia Whatsapp

Na kwakuwa naamini eBooks zangu zitakusaidia nakupa 7 Days 100% Money Back Guarantee

Zinunue, Zisome ndani ya siku 7

K**a haijakusaidia kabisa wasiliana na team yangu whatsapp 0742 112 946 tutakurudishia fedha yako yote.

24/07/2022

“Go through it but NEVER QUIT” - Kuna majira katika maisha huwezi kuyakwepa.

Ni majira ya MAUMIVU na UGUMU wa hali ya juu.

Ni yale majira ukiwa kitandani kwako unakosa usingizi na unasema...

“Nadhani sasa ndio basi tena, nimefika mwisho.

Niangalie kitu kingine hapa ndio basi tena”.

Huu ni wakati wa kawaida kwa kila mwenye ndoto kubwa.

Ni maumivu ya kawaida kwa mtu mwenye malengo makubwa.

Kuna maumivu mengine yatatokana na Makosa ambayo utakuwa umefanya mwenyewe.

Usiendelee kujihukumu, jisamehe, jifunze na fungua ukurasa mpya usonge mbele.

Huwezi kuinuka kwa kuendelea kulia na kusikitika.

Katika kipindi hiki unaweza kupata presha kubwa sana ya kulaumiwa kwa ulichofanya...
..kuchekwa kwa aibu iliyokukuta ama watu kukutolea mifano ya watu waliofeli katika jambo fulani.

Take heart and make one more step

(Jitia moyo na chukua hatua nyingine moja leo).

Una kitu kikubwa ndani yako na HATIMA yako ni kubwa sana.

Watu wenye hatima ndogo hawakutani na hizi changamoto kwa sababu ni k**a wanapanda mlima mdogo.

USIJILINGANISHE nao.

Wewe hatima yako ni k**a MLIMA MREFU sana unahitaji pumzi na njiani kuna kuchoka na kuhisi kuishiwa nguvu.

Don’t Quit!

Haya unayopitia leo yanakutengenezea USHUHUDA.

Yanakuimarisha na yanakujengea TABIA zinazohitajika kwa ajili ya mafanikio yako.

Be Strong!

Kesho yako Inang’ara kuliko jana na leo yako.

Be confident!

Chochote unachopitia leo, jiambie “Ingawa napitia magumu haya, SITAKATA TAMAA”-

Go through it but never Quit!

See You At The Top

19/07/2022

Kuna tabia mbili ukiwa nazo zinaweza kukupa stress sana...
..na kukuharibia mahusiano na watu ambao wangeweza kuwa msaada kwenye maisha yako.

Tabia ya kwanza ni kuwa na wivu wengine wanapoinuliwa.

Hii ukiiendekeza itakutesa sana.

Kwenye maisha yako, kila wakati lazima kuna watu watang’ara zaidi yako.

Lazima kuna watu watainuliwa kwenye maeneo yao zaidi yako...
..wapo ambao watasifiwa tu kuliko wewe.

Ukiwa mtu ambaye unaumia wengine waking’ara, itakutesa sana.

Utaishia kuwa mtu wa majungu na kuwasema vibaya wengine ambayo haitakusaidia.

Jifunze kukubali uwezo wa wengine.

Learn to Appreciate, Learn to Celebrate Others.

Jambo lingine ni kufanya vitu ili kushindana na wengine.

Kuna watu wengi wamepoteza mwelekeo wa maisha yao...
..kwa sababu ya kutaka kuprove kwa wengine kuwa wako juu zaidi yao.

Kuna watu wanatumia gharama kubwa sana na kupoteza rasilimali zao...
..ili tu kuonesha kuwa wako juu zaidi ya wengine.

Usisahau kuwa ni hasara kubwa kwenye maisha yako kushindana na mtu ambaye yuko kwenye wito wake.

Yaani, hata siku moja mwanadamu hawezi kushindana kuogelea na samaki, atajichosha tu.

Kaa eneo lako, fukuzia malengo yako.

Hivi sasa unaweza kuaccess VIDEO za kozi zangu zote 5 zilizopita.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi

2. Namna Ya Kujiajiri Kwa Mafanikio

3. Jinsi Ya Kutegeneza Fedha Kupitia Kipaji Chako

4. Jinsi Ya Kuondokana na Madeni

5. Money Formula

Thamani ya kozi hizi ni zaidi ya Tsh 170,000.00

Ila asubuhi ya LEO nitakupa ACCESS ya VIDEO ya kozi hizi zote kwa:

Tsh 9,999 Tu!

Kupata kozi hizi

Tuma Tsh 9,999 Tu!

Kwenda M-PESA

0762 312 117 (Joel Nanauka)

Kisha tuma UTHIBITISHO WA MUAMALA na neno "KOZI" kwenda

Whatsapp +255 762 312 117

Ndani ya masaa 24 utapatiwa utaratibu wa kupata access ya VIDEO za KOZI.

SHARE na mwingine ajifunze...

SAVE Post hii unaweza ihitaji siku za usoni.

COMMENT ulichojifunza hapa chini
👇

See You At The Top

Joel Arthur Nanauka.

14/07/2022

Kila mtu kwenye maisha yake huwa kuna kipindi anapitia kinaitwa “Wildernesss Season” (Majira ya Kuwa Jangwani).

Hiki ni mojawapo ya kipindi kigumu sana kwenye maisha.

Mara nyingi kwenye kipindi hiki huwa unajikuta unabakia peke yako...
..wale watu wa karibu ni k**a hauwaoni tena na ni K**a kwenye mambo mengi unakuwa hauna tumaini kabisa.

Watu wengi sana ndoto na malengo yao YAMEFIA KIPINDI CHA JANGWANI.

Kuna mahusiano mengi sana YAMEFIA kipindi hiki.

Majira haya, huwa yanaambatana na kutoona UWEZEKANO wa kuinuka tena...
..KUPATA FURAHA tena ama KUFANIKIWA TENA.

Kipindi hiki SAUTI yako ya Ndani huwa inakusemesha KUSHINDWA na kutokuwezekana tu.

Ni k**a KILIO na MACHOZI yako hakuna ANAYEYAJALI.

Mungu huwa anaruhusu upite kipindi kwa makusudi maalumu.

Huwa anataka UJIFUNZE kumtegemea yeye na sio wanadamu.

Huwa anataka kukuonesha kuwa Hata wengine wakikuacha yeye bado ANAKUJALI.

Wakati huu anautumia KUKUJENGA MISULI ya IMANI yako...
..ili utakapokabiliwa na CHANGAMOTO K**a hii huko mbeleni, UISHINDE.

Usikubali KUFIA JANGWANI, Tumaini lako liko njiani.

Hivi sasa unaweza kuaccess VIDEO za kozi zangu zote 5 zilizopita.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi

2. Namna Ya Kujiajiri Kwa Mafanikio

3. Jinsi Ya Kutegeneza Fedha Kupitia Kipaji Chako

4. Jinsi Ya Kuondokana na Madeni

5. Money Formula

Thamani ya kozi hizi ni zaidi ya Tsh 170,000.00

Ila asubuhi ya LEO nitakupa ACCESS ya VIDEO ya kozi hizi zote kwa:

Tsh 9,999 Tu!

Kupata kozi hizi

Tuma Tsh 9,999 Tu!

Kwenda M-PESA

0762 312 117 (Joel Nanauka)

Kisha tuma UTHIBITISHO WA MUAMALA na neno "KOZI" kwenda

Whatsapp +255 762 312 117

Ndani ya masaa 24 utapatiwa utaratibu wa kupata access ya VIDEO za KOZI.

SHARE na mwingine ajifunze...

SAVE Post hii unaweza ihitaji siku za usoni.

COMMENT ulichojifunza hapa chini
👇

See You At The Top

Joel Arthur Nanauka.

Address

Bukoba
Tegeta

Telephone

+255764426051

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Aden kisimbe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Aden kisimbe:

Share