MPAPA ze MOTO

MPAPA ze MOTO Film Director/Music Director
Video Shooting,Photoshooting
Graphic Disegner

Location tunatesti
09/05/2025

Location tunatesti

13/04/2025

AMRI KUMI ZA MAISHA YA NDOA…

1. USIJITENGENEZEE MAHUSIANO MENGINE YANAYOZIDI MAHUSIANO YAKO NA MWENZI WAKO: Pasitokee MTU mwingine (wa jinsia yeyote) ambaye atakuwa na umuhimu wa juu zaidi kuliko mwenzi wako.

2. USIMLINGANISHE AU KUMSHINDANISHA MWENZI WAKO NA MTU MWINGINE: Kumbuka kila mtu yupo tofauti. Tumia hekima kumfanya mwenzi wako awe bora zaidi pasipo kumfanya ajisikie kwamba hafai au hana viwango unavyotaka wewe.

3. USITUMIE “TENDO LA NDOA” K**A FIMBO YA KUMWADHIBU MWENZI WAKO: Hata k**a mmepishana misimamo, kumbuka “Tendo la Ndoa” ni haki ya msingi ya kila mwanandoa.

4. USIISHI MAISHA YA SIRI KWA MWENZI WAKO: Fanya jitihada za makusudi kuvunja kila tabia ya usiri ambayo itasababisha kila mmoja aishi maisha yake binafsi.

5. USIJILAUMU KUINGIA KWENYE NDOA AU KUMWONYESHA MWENZI WAKO KWAMBA UNAWEZA PATA MBADALA WAKE WAKATI WOWOTE ULE: Hata k**a unahisi “ulichemsha”, sasa fanya wajibu wako kuiboresha hiyo ndoa. Kumbuka UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.

6. USIRUHUSU KAZI AU MAJUKUMU YAKO YAIDHOOFISHE NDOA YAKO: Pamoja na majukumu mengi uliyonayo, hakikisha umuhimu wa ndoa yako unabaki palepale.

7. USIWE MBINAFSI: Usipendelee mambo yako tu au ndugu zako tu; bali kumbuka pia mwenzi wako anao upande wake.

8. USIWE MWEPESI KUSAMBAZA MAMBO YENU YA NDANI KWA KILA MTU: Ndoa ni taasisi yenye kanuni na taratibu zake; mojawapo ya kanuni hizo ni “utunzaji wa mambo nyeti” (Confidentiality). Uwe makini unamwambia nani kitu gani.

9. USIJIDANGANYE KWAMBA KUNA MTU MWINGINE ANAKUPENDA NA KUKUJALI ZAIDI YA MUME/MKE WAKO: Kumbuka kuna watu wataonyesha wanakujali sana kwa sababu sasa upo kwenye ndoa; siku ukitoka hutaamini k**a ndio wale!!

10. USISAHAU KIAPO CHA NDOA NI KIAPO CHA DAMU… NI KIAPO CHA MAISHA: Usiruhusu mawazo ya kutengana au kuachana yawe RAHISI na MEPESI sana ndani ya kichwa na moyo wako. Mara zote katika changamoto jikumbushe KIAPO CHA NDOA… “Nitakuwa nawe katika hali zote…!!”

NB:
- Paleka shida zako kwa MUNGU kabla hujazipeleka kwa MARAFIKI au WAPAMBE.

-

17/10/2023

1- KUOMBA KINGA YA NJAA NA KHIYAANA

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْجُوعِ فَإِنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخِيَانَةِ فَإِنَّهَا بِئْسَتِ الْبِطَانَةُ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-juw’iy fainnahu biisadhw-dhwajiy’u wa a’uwdhu bika minal-khiyaanati fainnahaa bi-isatil-bitwaanatu.

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na njaa kwani hiyo ni mbaya mno kulala nayo, na najikinga Kwako khiyana kwani hiyo ni dhamira ovu.
[Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Swahiyh An-Nasaaiy (3/1112

2- DUA YA KUOMBA AFYA NA RIZKI

اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي، وَارْحَمْـني، وَاهْدِنـي، وَاجْبُرْنـي، وَعافِنـي وَارْزُقْنـي وَارْفَعْـني

Allaahummagh-fir-liy warhamniy, wahdiniy, wajburniy, wa ‘aafiniy, warzuqniy, warfa’-niy

Ee Allaah, nighufurie, na nirehemu, na nihidi na niunge kunitengenezea niliyoharamika nayo, na nipe afya, na niruzuku, na nipandishe [daraja].
(Sunan)

3- DUA KUOMBA RIZIKI

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ عِلْمًا نَافِعًا وَرِزْقًا طَيِّبًا وَعَمَلاً مُتَقَبَّلاً

Allahumma inni as’aluka ‘ilman nafi’an, wa rizqan tayyiban, wa ‘amalan mutaqabbalan

Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba elimu yenye manufaa, riziki njema na vitendo vinavyokubalika.’

Sunan Ibn Majah 925

______

16/10/2023

🌹🌹 *ASSALAAM ALEYKUM WARAHMATULLAAHI WABARAKAATUH* 🌹🌹

Yaa *ALLAAH* Tunashukuru kwa Rehma zako na Mapenzi yako umetujalia tumeweza kudiriki kuiona siku ya Leo

Yaa *ALLAAH* Tunakuomba utupe Afya na Siha Njema sisi pamoja na Familia zetu .

Yaa *ALLAAH* Tunakuomba Uwajalie heri Wazazi wetu na waliotangulia mbele ya haki tunakuomba uwaepushe na adhab zako.

Yaa *ALLAAH* Tunakuomba utukunjulie Riziki zetu ,utujalie Umri mrefu wenye Manufaa nasi.

11/10/2023

WAFU WANATAMBUAJE KUWA WAMEKUFA?

!!!

Mtu aliyekufa hatambui kwamba alikufa mwanzoni. Anajihisi anaota kifo, anajiona analia, anaoga, anajipiga magoti na kushuka kaburini.

Kila mara huwa na hisia ya kuota anaporundikana ardhini. Kisha hupiga mayowe lakini hakuna anayesikia kilio chake.

Baadaye, kila mtu anapokuwa ametawanywa na kuachwa peke yake chini ya ardhi, Mwenyezi Mungu huirejesha nafsi yake. Anafungua macho yake na kuamka kutoka kwenye "ndoto yake mbaya". Mwanzoni anafurahi na kushukuru kwamba yale aliyokuwa akipitia yalikuwa ndoto tu, na sasa. yuko macho kutoka usingizini. Kisha anaanza kuugusa mwili wake, ambao ndio kwanza umefungwa kwa kitambaa, akiuhoji kwa mshangao.

"Shati yangu iko wapi, chupi yangu iko wapi?"

Kisha anaendelea: "Niko wapi, mahali hapa ni wapi, mbona harufu ya uchafu na matope kila mahali, ninafanya nini hapa?"

Kisha anaanza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi, na kile anachopata sio ndoto! Ndio, aligundua kuwa alikuwa amekufa kweli.

Anapiga kelele kwa sauti kubwa iwezekanavyo, anaita: jamaa zake ambao, kulingana na yeye, wangeweza kumuokoa:

"Razaq...!!!!"
"Oyiza.... !!!!"
"Abdullahi.... !!!!"
"Khadijah....!!!!"
"Aisha....!!!!"
"Uthman....!!!!"
"Adam....!!!!"
Hakuna anayemjibu. Kisha anakumbuka kwamba Mwenyezi Mungu ndiye tumaini pekee hivi sasa. Anamlilia na kumsihi huku akiomba msamaha Wake; Yah Mwenyezi Mungu! Yah Allah!! Nisamehe Yah Allah...!!!

Anapiga kelele kwa hofu ya ajabu ambayo hakuwahi kuhisi hapo awali, wakati wa uhai wake.

Ikiwa yeye ni mtu mzuri, malaika wawili wenye uso wa tabasamu watamketisha chini ili kumfariji, kisha wamfanyie huduma bora zaidi.

Ikiwa yeye ni mtu mbaya, Malaika wawili watamzidishia khofu na kumtesa kulingana na matendo yake maovu.

Ee Mwenyezi Mungu, nisamehe dhambi zangu na dhambi za mama yangu, baba yangu, mke wangu, watoto wangu na jamaa zangu na marafiki zangu wote.

Kaka na dada katika Uislamu, mna chaguzi mbili hapa:

1. Ujuzi huu mdogo usomeke hap

HUKUMU YA MWENYE KUFANYA DHAMBI KUBWA. Mwenye kufanya Dhambi Kubwa, isiyokuwa Shirki au ukafiri, hatoki katika Uislamu k...
02/09/2022

HUKUMU YA MWENYE KUFANYA DHAMBI KUBWA.

Mwenye kufanya Dhambi Kubwa, isiyokuwa Shirki au ukafiri, hatoki katika Uislamu kwa dhambi hiyo. Hapa duniani anakuwa Muislamu mwenye imani pungufu. Ni Muislamu kwa imani yake na ni fasiki (muovu) kwa dhambi yake kubwa, na huko akhera atakuwa katika utashi wa Allah. Akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu. Akiadhibiwa hatokaa milele motoni, bali atatoka motoni humo kwa ile imani aliyonayo, hata k**a ni chembe ndogo kabisa. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) isemayo kuwa:

“Atatoka motoni yeyote aliyetamka «Laa ilaaha illa Allah» = Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu na ilhali moyoni mwake kuna kheri japo k**a uzito wa punje ya shairi. Na atatoka motoni yeyote aliyetamka Laa ilaaha illa Allah = Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu na ilhali moyoni mwake kuna kheri japo k**a uzito wa punje ya ngano. Na atatoka katika moto yeyote aliyetamka Laa ilaaha illa Allah = Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu na ilhali moyoni mwake kuna kheri japo yenye uzito wa chembe ndogo kabisa”.

Hadithi hii imesimuliwa na Bukhari na Muslim.

  Video
17/05/2021

Video

KARIBU TUKUHUDUMIE....0694 176 636

30/04/2021

Address

Tanga

Telephone

0657979339

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MPAPA ze MOTO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MPAPA ze MOTO:

Share

Category