Tanga Tanzania

Tanga Tanzania Mpiga picha kutoka mkowa wa Tanga, karibu Tanga Tanzania
(5)

08/08/2026

madiwadi wa Handeni wametembelea banda la Tanga jijini katika maonesho ya Nane Nane 2026 kanda ya mashariki mkoa wa morogoro

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Tanga katika ...
08/08/2026

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Tanga katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro, na kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji, ubunifu na maendeleo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Kikwete aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge.

Viongozi hao walitembelea banda hilo na kupokea maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji, shughuli za uzalishaji, huduma za kijamii pamoja na mikakati ya Jiji la Tanga katika kukuza uchumi na kuboresha mazingira ya biashara.

Banda la Tanga linaonesha fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta za viwanda, biashara, utalii, uvuvi na huduma, likiwa sehemu ya jitihada za kuitangaza Tanga k**a kitovu cha uwekezaji na biashara nchini.

Ushiriki huo unaendana na kaulimbiu ya Maonesho ya Nane Nane mwaka 2026 isemayo, "Tambua soko, ongeza tija, tekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," kwa kuhamasisha matumizi ya ubunifu na teknolojia katika kuharakisha maendeleo ya uchumi.

07/08/2026

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.batilda burian Akimkabidhi Mhe.rais mstaafu Kikwete. Zawadi/ bindaa zilizo tengenezwa na mjasiriamali kutoka jijini Tanga katika Maonyeshe ya nanenane yanayo fanyika kanda ya mashariki mkoa wa morogoro.

07/08/2026

Wajasiriamali kutoka kata ya Chongoleani, na mabokweni kupitia mradiwa wakiwa katika banda la Tanga jiji, kwenye Maonyeshe ya nanenane yanayo fanyika kanda ya mashariki mkoa wa morogoro.

07/08/2026

Maonyeshe ya nane nane yanayo fanyika kanda ya mashariki mkoa wa morogoro. Karibu katika banda la

Dr. Hassan Mshinda, Mshauri wa  Ametembelea banda la Tanga jiji na kujionea bidha mbalimbali zilizo tengenezwa na wajasi...
07/08/2026

Dr. Hassan Mshinda, Mshauri wa Ametembelea banda la Tanga jiji na kujionea bidha mbalimbali zilizo tengenezwa na wajasiriamali mbalimbali kutoka jiji la Tanga katika Maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika Morogoro.

06/08/2026

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kupokea vipande 17,006 vya reli na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya takribani Dola milioni 56 za Marekani.

Amesema, uwekezaji huo utaongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo, kuchochea biashara na kukuza uchumi wa Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Balozi Dkt. Batilda amesema, Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya reli ili kuongeza uwezo wa usafirishaji wa mizigo na abiria, huku maboresho ya reli ya Kaskazini yakilenga kuongeza kasi ya treni, kubeba mizigo mizito na kuimarisha huduma inayounganisha Bandari ya Tanga na mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Ameongeza kuwa uwekezaji huo unaenda sambamba na utekelezaji wa miradi ya Reli ya Kisasa (SGR) inayolenga kuimarisha mtandao wa reli nchini na kufungua fursa zaidi za biashara na uwekezaji.Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wananchi kushiriki katika kulinda miundombinu ya reli, na mali nyingine za umma kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola dhidi ya vitendo vya uharibifu.

Kwa upande wake, Meneja wa TRC Kanda ya Tanga, Christopher Kalisti, amesema reli mpya zitachukua nafasi ya reli za zamani zilizokuwa zikisababisha vizuizi vya mwendo, hivyo kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na abiria.

Amesema, kipande kinachoboreshwa kinaunganisha reli ya Kaskazini kutoka Bandari ya Tanga kuelekea Kilimanjaro na Arusha, na reli ya Kati, na kuwa kiungo muhimu cha biashara na usafirishaji.

Naye Meneja wa Bandari ya Tanga, Salehe Mbega, amesema maboresho ya reli yataongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia shehena zinazoelekea Rwanda, Burundi na nchi nyingine za Afrika Mashariki, hatua itakayoongeza kasi ya utoaji wa mizigo na kuimarisha ushindani wa Bandari ya Tanga.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) ...
06/08/2026

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa nishati na kuifanya Tanga kuwa kitovu cha nishati cha kikanda.

Utiaji saini huo umefanyika leo Agosti 6, 2026 Ikulu, Dar es Salaam. Hati ya makubaliano iliyosainiwa ni kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC), pamoja na kampuni ya kimataifa inayojihusisha na nishati na biashara ya bidhaa ghafi, Vitol Bahrain E.C ya nchini Uholanzi.

Makubaliano hayo yanaendana na jitihada za kuimarisha nafasi ya Tanzania katika sekta ya nishati kupitia miradi ya kimkakati ikiwemo Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), linalounganisha maeneo ya uzalishaji wa mafuta ghafi Hoima nchini Uganda na Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mradi wa EACOP unalenga kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi kwenye masoko ya kimataifa kupitia Bandari ya Tanga, huku ukiwa na umuhimu mkubwa katika kukuza biashara, uwekezaji, ajira na maendeleo ya miundombinu katika nchi hizo mbili.

Kupitia utekelezaji wa EACOP na miradi mingine ya nishati, Bandari ya Tanga inatarajiwa kuimarika zaidi na kuwa kitovu cha kimkakati cha nishati kwa ukanda wa Afrika Mashariki, sambamba na kuongeza uwezo wa Tanzania kuhudumia mahitaji ya nishati ya kikanda.

Maonyeshe ya nane nane yanayo fanyika kanda ya mashariki mkoa wa morogoro. Karibu katika banda la Tanga jiji kujipatia b...
06/08/2026

Maonyeshe ya nane nane yanayo fanyika kanda ya mashariki mkoa wa morogoro. Karibu katika banda la Tanga jiji kujipatia bidhaa mbalimbali

Address

Mikanjuni
Tanga
122

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanga Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share