TANGA MEDIA

Directions

TANGA MEDIA TANGA MEDIA ONLINE
(1)

11/10/2026

Nyd de videoer og den musik, du holder af, upload originalt indhold, og del det hele med venner, familie og verden på YouTube.

Mrembo wa Tanzania, Jihan Dimack ameibuka mshindi wa taji kuu la Miss Grand International 2026 katika fainali ya mashind...
10/10/2026

Mrembo wa Tanzania, Jihan Dimack ameibuka mshindi wa taji kuu la Miss Grand International 2026 katika fainali ya mashindano hayo iliyofanyika leo, Oktoba 10, 2026, Jijini Bangkok, Nchini Thailand.

Kwa ushindi huo, Jihan Dimack ameandika historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa Taji Kuu la Miss Grand International tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 2013.

10/10/2026

JIHAN MISS NAMBA 1 GRAND INTERNATIONAL

10/10/2026

JIHAN AINGIA TOP 5 MISS GRAND INTERNATIONAL

10/10/2026
Miss Grand Tanzania Jihan Dimack amevunja rekodi  ya kupata  maoni mengi zaidi Instagram kupitia chapisho lililowekwa  k...
10/10/2026

Miss Grand Tanzania Jihan Dimack amevunja rekodi ya kupata maoni mengi zaidi Instagram kupitia chapisho lililowekwa katika ukurasa wa Miss Grand International.

Chapisho hilo limepata maoni milioni 149 hadi sasa, ikiwa ni mwitikio mkubwa wa watumiaji wa Instagram wakati wa mashindano hayo.

Idadi hiyo inaifanya posti hiyo kuingia kwenye rekodi ya machapisho yaliyopata komenti nyingi zaidi kwenye mtandao huo huku akiwapiku mastaa wakubwa waliowahi kutikisa katika orodha hiyo.

Utakumbuka, orodha iliyochapishwa na CommentGrid Septemba 22, 2026
machapisho yenye komenti nyingi moja wapo ni la Alexandros Kopsialis, lililokusanya takribani komenti milioni 43.2, huku la mwanamuziki Bizarrap akimshirikisha Paulo Londra likiwa na takribani milioni 21.8.

Chapisho jingine ni la marehemu ###Tentacion, lenye takribani komenti milioni 10.8, na lile la Lionel Messi akisherehekea ushindi wa Argentina katika Kombe la Dunia la 2022.

Idadi ya komenti kwenye posti ya Jihan inaendelea kuvutia kutokana na mwitikio wa watumiaji wa Instagram, huku mashabiki wa mashindano ya urembo wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa washiriki wanaowania taji la Miss Grand International.

Aidha wingi wa komenti hiyo unakuja ukiwa ni muendelezo wa upigaji kura unaoendelea ambao unatarajia kutamatika hii leo.

Moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Miembeni B, Kata ya Magaoni, jijini Tanga, umeteketeza mabanda...
09/10/2026

Moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Miembeni B, Kata ya Magaoni, jijini Tanga, umeteketeza mabanda 17 ya wafanyabiashara wa mbao na mafundi seremala, na kusababisha hasara kubwa ya mitaji, bidhaa na vifaa vya kazi.

Waathirika wamesema moto huo ulisambaa kwa kasi kutoka banda moja hadi jingine kutokana na uwepo wa mbao na vifaa vinavyoshika moto kwa urahisi, hali iliyofanya juhudi za kuokoa mali zao kushindikana na kusababisha baadhi yao kupoteza mali zenye thamani ya mamilioni ya fedha.

Mmoja wa waathirika, Shaban Mmari, amesema alikuwa ameingiza mzigo wa mbao wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 40, lakini mali zake zote zimeteketea, huku Edward Petro, aliyekuwa akifanya biashara katika eneo hilo tangu mwaka 2019, akisema amepoteza mashine za mbao na vifaa vingine vya kazi.

Kutokana na janga hilo, waathirika wameiomba Serikali pamoja na wadau wengine kuwasaidia kuanzisha upya biashara zao, wakieleza kuwa wamepoteza mitaji na vyanzo vyao vya mapato huku baadhi yao wakikabiliwa na madeni na kushindwa kutimiza oda za wateja.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Gilbert Kalima, amesema tathmini ya jumla ya hasara ilikuwa haijakamilika na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku akieleza kuwa uchunguzi unaendelea na Serikali itaendelea kushirikiana na waathirika katika kipindi hicho kigumu.

09/10/2026

Mmoja wa majeruhi wa ajali iliyoua watu 28 katika eneo la Mkambarani mkoani Morogoro, Mohamed Abdalah amesimulia namna ajali hiyo ilivyotokea.

Aidha katika hatua nyingine, Meneja wa Kampuni ya Basi la Green Line lililoteketea kwa moto, Chubura William amesema katika ajali hiyo, wafanyakazi wanne wa basi hilo wamefariki dunia.

Address

Mikanjuni
Tanga
122

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TANGA MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share