05/07/2023
Jinsi Mchungaji Alivyoiba hundi(cheque) ya Benki ya $ 25,000.00 Wakati wa Chakula cha jioni katika Nyumba ya Mwanachama
Wanandoa katika kanisa flan walimwalika Mchungaji wa Kanisa lao kwa chakula cha jioni nyumbani kwao.Mchungaji alifurahi Sana na alipomaliza kula, basi akenda zake nyumban kwake.
Ila Baada ya Mchungaji kuondoka, wenzi hao waligundua hundi(cheque) yao imepotea. Mtu huyo alimwambia mkewe; "Nadhani Mchungaji ameiba hundi ya benki iliyo wazi ya $ 25,000.00 ambayo niliiweka hapa kwenye meza ambayo nilikuwa na nia ya kumpa".
Kwa hasira mkewe akasema; “Hmmmm! Wote ni sawa tu. Ikiwa ni wezi, matapeli. Hakuna haja ya kumwalika tena, tokea sasa tutahudhuria Kanisa lingine ”.
Miezi miwili Baadaye, mwanamke huyo alikutana na Mchungaji huyo kwenye barabara fulani na alikuwa na ujasiri wa kutosha kumkabili na akasema: “Habari za asubuhi Mchungaji, umegundua kuwa hatuji Kanisani tena, hii ni kwa sababu tumekukasirikia. Ile Siku uliyokula nyumbani kwetu, kulikuwa na hundi ya benki ya $ 25,000.00 mezani lakini kwa bahati mbaya ilipotea wakati tunakula. Wewe ndiye Mtu pekee uliyezuru nyumba yetu wakati huo ”.
Mchungaji akamwambia, “Ndio, nilichukua hundi hio Nikaiweka ndani ya Biblia yako ili kuepuka kuimwagia mchuzi ”.
Mwanamke huyo alichanganyikiwa sana na akalia huku akimsihi Mchungaji amsamehe.
Kurudi nyumbani kwake, alichukua Biblia na kupata hundi ya benki ambayo ilikuwa imekaa kwa miezi miwili.
Hii ilimaanisha kuwa kwa miezi miwili, alikuwa hajaifungua biblia yake. Kwa miezi miwili, yeye na mumewe walimshtaki Mchungaji asiye na hatia. Kwa miezi miwili, tukio hilo lilikuwa likiwatesa bila sababu.
Ni mara ngapi tunashuku na kuwashtaki watu wengine bila uthibitisho wa kweli, ushahidi au ushuhuda?
Ni mara ngapi unampa mtu jina baya ?
Ni mara ngapi unatafsiri vibaya matendo ya kaka au dada ambayo wao walikua hawana Nia mbaya kwako?
Somo: ikiwa unafikiria ndugu yako amekukosea..mwambie .... muulize ... Mrekebishane kwa upendo.... usiweke kinyongo cha bure.
•Nawapenda sana ndugu zangu