iam_bisher

iam_bisher Iconic Photographer | The Camera Hub
(1)

23/05/2026
SERIKALI YAENDELEA NA MPANGO WA KUANZISHA KONGANI ZA VIWANDA SINGIDA Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kuanzisha...
16/05/2026

SERIKALI YAENDELEA NA MPANGO WA KUANZISHA KONGANI ZA VIWANDA SINGIDA Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kuanzisha Kongani za Viwanda katika wilaya zote nchini, ikiwemo Mkoa wa Singida, kwa lengo la kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi. Hayo yamesemwa Mei 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), akijibu Swali namba 356 la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Mhe. Grace Elias Mkoma aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kuanzisha Kongani za Viwanda kwa Wilaya za Mkoa wa Singida. Amesema hadi kufikia Desemba 2025, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imefanikiwa kuanzisha Kongani 36 za Viwanda katika Mikoa 16 nchini, hatua inayolenga kuongeza uwekezaji wa Viwanda pamoja na kuchochea maendeleo ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. Akijibu Swali hilo, Londo amesema tayari maeneo yametengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida. Ametaja maeneo hayo kuwa ni Singida Manispaa yenye ekari 8.6, Manyoni ekari 4.7, Iramba ekari 20, Itigi ekari 10 pamoja na Mkalama ekari 10.

SERIKALI KUJENGA KIWANDA CHA SARUJI HANANG Serikali imesema inatafuta Mwekezaji wa uhakika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwand...
11/05/2026

SERIKALI KUJENGA KIWANDA CHA SARUJI HANANG Serikali imesema inatafuta Mwekezaji wa uhakika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, kwa kuwa kuna malighafi za kutengeneza Saruji. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb) Mei 11, 2026 Bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akijibu Swali namba 305 la Mbunge wa Hanang Mhe. Asia Halamga, aliyetaka kujua Mpango wa Serikali wa kuanzisha Kiwanda hicho kutokana na uwepo wa malighafi za kutosha Wilayani humo. Akijibu Swali hilo, Naibu Waziri Londo amesema Serikali inatambua uwepo wa malighafi zinazotumika kuzalisha Saruji katika Wilaya ya Hanang’ na tayari imeweka mazingira ya utekelezaji wa mradi huo. Amesema Serikali imetenga eneo la ekari 360 kwa ajili ya mradi huo, ambapo ekari 300 ni eneo lenye malighafi huku ekari 60 zikitengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda huku hatua za kutafuta Mwekezaji zikiendelea ili kuhakikisha ujenzi wa Kiwanda hicho unaanza na kusaidia kukuza uchumi wa eneo hilo pamoja na kuongeza ajira kwa Wananchi. Londo amefafanua kuwa mkakati huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, inayosisitiza ujenzi wa Viwanda vya kimkakati kulingana na rasilimali zilizopo katika kila Mkoa. Amebainisha kuwa mbali na Saruji, Hanang’ ina utajiri wa malighafi za uzalishaji wa Chumvi pamoja na fursa kubwa katika zao la Ngano, maeneo ambayo Serikali inayaandaa kwa ajili ya uwekezaji wa kuongeza thamani ili kuimarisha soko la ndani na nje ya nchi. Katika hatua nyingine, ameeleza kuwa mpango wa kuimarisha Viwanda hautaishia Hanang pekee, bali unahusisha pia Wilaya ya Babati na maeneo mengine nchini kupitia uanzishwaji wa kanda maalum za uwekezaji kwa lengo la kuongeza thamani, kukuza mauzo ya nje, na kupaisha uchumi wa Wananchi kulingana na vipaumbele vya Kitaifa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (Kulia), Mhe.  Dennis Londo (Mb) akisalimiana Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambi...
07/05/2026

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (Kulia), Mhe. Dennis Londo (Mb) akisalimiana Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambia, Mhe. Njavwa Simutowe (Mb) kabla ya kuanza Mkutano wa Mawaziri wa Biashara (Joint Trade Committee - JTC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zambia Mei 7, 2026 katika Kituo cha Huduma cha Pamoja Mpakani (OSBP) mjini Tunduma mkoani Songwe.

KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027.Kamati ya Kudumu ya...
26/03/2026

KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027.Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), imeridhia Randama ya mpango wa bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Machi 26, 2027 Bungeni jijini Dodoma.

Ujana safi na kumcha Mungu πŸ™
16/03/2026

Ujana safi na kumcha Mungu πŸ™

πŸ“πŸ˜
09/02/2026

πŸ“πŸ˜

06/02/2026
Bisher 🫰
04/12/2025

Bisher 🫰

Address

Mikumi Morogoro
Mikumi
255

Telephone

+255674756975

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when iam_bisher posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to iam_bisher:

Share

Category