abbi madboe

abbi madboe Football ⚽ for everyone best enjoyment is football ⚽⚽

07/09/2024

07/09/2024

Watu 12 wakiwemo Watoto wawili wamefariki na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya, ajali hiyo imetokea leo ljumaa September 06,2024, baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameiambia kuwa “Basi liliacha njia kwenye kona kali kwenye mteremko mkali na kugonga gema na kupinduka na kusababisha vifo vya Watu 12 (Wanaume watano, Wanawake 7) miongoni mwao Watoto wadogo wawili, na kusababisha majeruhi ya Watu zaidi ya 36 ambao wenye hali mbaya ni watano”

“Kuna Watoto wameachwa mpaka sasa hivi Wazazi wao wamefariki, ni Watoto wa miezi sita hadi miezi nane, tunaendelea kufanya mawasiliano na Ndugu wa Marehemu maeneo ya Tabora, Mbeya na maeneo mengine kwasababu kote kuna Watu ambao walikuwa wanasafiri”

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi, Dereva alianza kwa kasi kubwa akitokea Mbeya kwenda Tabora alipita kona zote ngumungumu kabla hajafika kona ngumu ya mwisho mizigo ikaanza kudondoka kwenye gari baada ya buti ya gari kufunguka, Kijana mmoja ambaye sasa ni Marehemu akatoa taarifa mizigo inaanguka, gari likasimama wakapakia mizigo”

“Wakiwa pale mabasi mawili yakawapita yakiwa yanaenda Tabora huwa wanakimbizana njiani kutafuta abiria, kwahiyo alipomaliza kupakia akaanza kukimbia tena kufika kwenye kona gari ikamshinda bampa la juu likakatika ikaanza kuwaburuza vichwa vikawa vinaburuzika”

07/09/2024

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amemtaka aliyekuwa Kada wa Chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa kumlipa kiasi cha shilingi Bilioni tano k**a fidia kwa madai ya kumtolea maneno ya kashfa.

Peter Msigwa ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA June 30 2024, amethibitisha kupokea barua kutoka kwa Jopo la Mawakili watano wa Mbowe ambapo katika wito huo wa barua iliyotolewa Septemba 2, 2024 miongoni mwa hoja kuu ni kwamba, mara baada ya Msigwa kujitenga na CHADEMA aliibua chuki hadharani na kwa ukaidi akatoa kauli zisizo za kweli, za uongo, nia mbaya na za makusudi dhidi ya Mteja wao (Mbowe).

Katika barua hiyo imebanisha kwamba maneno hayo ni ya kashfa ambayo yalisikilizwa na mamia ya Watu waliohudhuria mikutano mbalimbali iliyofanyika katika maeneo tofauti aliyokuwa ukihutubia ambayo yalitangazwa zaidi au kuchapishwa katika Vyombo vya Habari tofauti, vikiwemo magazeti na vyombo vya habari vya kielektroniki.

Inaelezwa kwamba Julai 19, 2024 Msigwa akiwa eneo Mwembetogwa alisema ya kwamba “Mh. Mbowe anatumia sekretarieti ya Chama kwenye Ofisi binafsi, anakitu kinaitwa Mbowe Foundation na hii ni kinyume na taratibu, huwa mnasikia Nyerere Foundation, Mkapa Foundation, Kikwete foundation, mshawahi sikia Samia Foundation? Foundation huwa zinaanzishwa ukishatoka madarakani, kwasababu hutakiwi kuwa na masilahi nazo, yeye ameanzisha kitu kinaitwa Mbowe Foundation, michango yote badala iende kwenye Chama inakuwa channelled kwenda Mbowe Foundation, kwenye account ya Chama pesa haziendi”.

🤩
07/09/2024

🤩

Rais alisema wakati alipoingia madarakani mwaka 2022 kwamba hakuna haja kwa viongozi wa Afrika kujikusanya wote kwenda kwenye mikutano ya kilele inayoandaliwa na mataifa yenye uwezo, na kupendekeza wawe wanawakilishwa na mtu mmoja tu! Mtazamo wa mchoraji wetu .

06/09/2024
06/09/2024

TAARIFA KWA UMMA.

06/09/2024

Mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Cosmopolitans FC utaonyeshwa leo Saa 10:00 kamili Jioni kupitia Yanga SC APP📲

Mwananchi Download na Lipia Yanga SC APP🔰👊🏽


06/09/2024

… Cristiano Ronaldo has scored his 𝟗𝟎𝟎𝐭𝐡 𝐜𝐚𝐫𝐞𝐞𝐫 𝐠𝐨𝐚𝐥 for club and country! 🇵🇹 The GOAT 🐐🔥🙌🏽

Address

Soweto
Mbeya
MBEYATOWN

Telephone

+255783081811

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when abbi madboe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to abbi madboe:

Share

Category