06/04/2019
Sehemu ya 36(The flight to Los Angeles) created by ASELI GB (Norman Johnz)
Endelea nayo
Basi Victoria alimnyanyua Traves halafu akamfuta machozi kwa mikono yake Kisha akasema "I'm sorry Traves"(samahani Traves) akawa anaondoka zake, Traves alilia K**a mtoto mdogo sababu hakuamini kilichotokea,alidiriki hata kuvunja mahusiano yake na Shirley kwa ajili ya Victoria matokeo yake Victoria naye amemuacha,Traves aliumia sana aliona K**a maisha yake yameharibika tayari.Siku zilisonga mbele, baada ya wiki tatu ndoa ya Trevor na Victoria ilianza kutayarisha, Trevor alikuwa amekwisha pona majeraha yake yote, Victoria alialika ndugu na jamaa kutoka Hawaii wahudhurie harusi hiyo pia mama yake naye alialika ndugu wa Kule ufilipino wahudhurie harusi hiyo, Trevor na Victoria walifurahi sana sababu ilikuwa Ni siku maalumu kwao lakini kwa traves ilikuwa Ni siku ngumu kwake sababu mwanamke ampendaye anafunga ndoa na pacha wake,siku ya harusi ilipofika Traves hakutaka hata kuhudhuria harusi hiyo,Basi harusi ilifanyikia palepale nyumbani kwa Gabriella sababu nyumba ilikuwa na eneo kubwa, hivyo ilikidhi mahitaji ya sherehe hiyo, baada ya Trevor na Victoria kuvishana Pete walielekea ufukweni, walifurahi huku wakipiga picha za ukumbusho wa ndoa hiyo baada ya hapo walirejea nyumbani mida ya saa mbili usiku.kesho yake mama yake Victoria alipanga ampeleke mwanaye ufilipino ili akamuoneshe kaburi la baba yake mzazi lakini kabla ya kuondoka ujumbe alioucha Traves ulikutwa ndani ya nyumba, Traves aliandika ujumbe ufuatao
"Congratulations bro, congratulations Victoria, I'm really happy and proud of your wedding cause it's a special event for you and even for me.the thing that I want to say is that I wish you a joyful life,may be you'll never see me again cause I've traveled to Sydney, Australia
I love you bro,I love you Victoria good luck, your brother and brother in law TRAVES MANUEL WI******ER.
(Hongera Kaka,hongera Victoria,ninafuraha na ninajivunia ndoa yenu sababu Ni tukio maalum kwenu na hata kwangu, Jambo ninalotaka kusema Ni kwamba nawatakia maisha yenye furaha tell,pengine hamtaweza kuniona Tena sababu nimesafiri kuja Sydney, australia.nakupenda Kaka, nakupenda Victoria,Ni Mimi Kaka na shemeji TRAVES MANUEL WI******ER
Trevor alivyoisoma barua hiyo alienda kumpatia mke wake ambaye Ni Victoria baada ya Victoria kuisoma Trevor alimpelekea mama yake,lakini mama yake alitambua Kila kitu sababu kabla ya Traves kuondoka alimuaga mama yake itaendelea....