27/09/2017
MTAA WA TATU (22)
(chombezo)
Age 18
By_____>Hafidhi j Ikram
Whatsapp_____>0675082390
/////////////////////-------------------
Tulipoishia
Jana
Zuwena hakuweza kuamini macho yakamtoka pima
Baada kukuta miili ya maafande imelaliana hovyo
wakiwa hawana tena uhai
si afande Ngogo wala nani wote wamechinjwa,
Wananchi walijazana na kuanza kuulizana
“hii imekuwaje polisi wote hawa wameuwawa"...
“yani sijui nisemeje
Polisi walikuwa sijui wanatokea wapi,
Sasa wakati wanapita hapa kuna kijana mmoja hivi shalobaro tu akapishana nao
Ghafla bin vuu yule sharo akaanza kutembeza kichapo kwa maafande wale. Mi nilijuwa bongo movie kumbe wanapigana kweli yule sharo alikuwa na visu k**a viwili.
Basi akatumia hivyo kuwachinja,
Nikaitoa simu yangu kushort video nikashort,
”embu tuone hiyo video"
Mimi nitumie whatsapp kaka"
Baada jamaa kusema kashort tukio zima kila mmoja akata aone mwingine atumiwe
Jamaa akasema
“ningewatumia tena mngeona tatizo yule sharo kasepa na simu yangu
kudadeki zake kanipiga zinga la mtama, na kuniambia
“lete simu lasivyo nitakuuwa.
Nikaona mmh!
Nisije kuchinjwa bure nikampa mwenyewe"
Zuwena hakuwa na jinsi zaidi ya kuitoa simu yake na kumpigia
Hafidhi majibu yakaja simu ya
mteja unaempigia haipatikani kwa sasa
jalibu tena baadae.
Zuwena akachoka hoi akamuuliza yule kijana aliyekuwa akisimulia tukio zima
“wee kaka umesema huyo
muuwaji kaondoka na simu yako?"
“ndio Dada yangu yani dahaa
simu nimeinunua juzi tu shilling laki
nane jamaa kaibeba"
jamaa akaongea hivyo huku machozi yakianza kumtoka,
“basi usilie nipe number ya simu yako
niweze kumpigia"
Jamaa akataja number za simu
Zuwena akapiga kwa bahati nzuri simu inaita.
Zuwena akaenda mbali kidogo na pale
huku akisikilizia k**a simu itapokelewa
ni kweli simu ikapokelewa
na wakati huohuo defender za polisi
k**a sita hivi zinaingia polisi
wakaruka kutoka kwenye magari yao
na kulizunguka eneo zima,
Afande mmoja akainama ulipolala mwili wa afande Ngogo na kuokota kitu k**a
kikaratasi hivi,
Akakifungua kilikuwa kidogo sana sema kikawa kikubwa baada kukikunjua
“nafahamu fika ni jinsi gani
mtakuwa na simanzi baada kuwauwa panya wenzenu. Naomba mtambuwe kitu kimoja
mwisho wa mchezo huu
mtakuja kupata matokeo. Nyie endeleeni
kuk**ata vibaka wezi
pigeni watu wenye kufanya maandamano
Msitake kuingia kwenye mkono
wa Mtaa wa tatu mimi ni zaidi ya chatu
nang'ata natafuna nameza.
Yeyote atakae nifatilia lazima auwawe"...
Barua ikaisha hivyo
“Aisee afande Agnes
inaonekana huyu jamaa anajiamini sana mpaka anafikia hatua ya kuitisha serikali"
“ndio maana yake sema muache aneng'eneke (One day) ipo siku moja tutamnasa tu ndio atajuwa kuwa serikali ina mkono mrefu
pumbavu zake"
Afande Agnes akaongea kwa hasira.
Zuwena nae akaisikilizia simu mpaka ikakata.
Na kuamua kupiga tena hatimae ikapokelewa
“Zuwena nini shida? nini tatizo?
Unataka kitu gani kwangu please tulia nyumbani usinipigie simu wala usitake kufahamu wapi nilipo
ukidadisi sana nawe utauwawa!"
Hafidhi aliongea hivyo kwa sauti ya ukali kisha akakata simu,
Habari zikatangazwa kila kona ya nchi
baada muuwaji kufanya
mauwaji mengine tena safari hii ya kutisha
Zaidi kauwa maafande kumi
watano kituoni
watano waliotoka kumtafuta wakakutana nae njiani akawachinja wote
kijana mwenyewe picha yake ni hii.
Ni kijana mdogo sana sema mambo yake ni hatari tupu"
“Toba"...nini hiki (Why)?
mama Hafidhi nini mwanao anafanya, hii ndio kazi aliyopewa na Ankor wake sio?
Niambie mke wangu kwanini mwanetu anauwa kipi kimemsibu?"
Mzee J Ikram aliongea kwa jazba kubwa baada kuona taarifa ya habari kuwa mwanae ameuwa tena polisi kumi.
Mkewe hakujibu kitu akabaki kulia tu
maana Hafidhi ndio mtoto
wa pekee leo hii kageuka kuwa muuwaji
itakuwaje k**a akik**atwa hukumu yake ni kunyongwa au kufungwa kifungo cha
Maisha jela.
“hapana siwezi kumuacha mwanangu
ateketee kwa mambo k**a haya
lazima nifanye kitu aisee"...
Akaitoa simu yake na kumpigia sijui nani
sauti upande wa pili ikasikika
“halloo mzee shikamoo vipi wazima huko?"
“marhabaa kijana wangu
Dennis kiupande wetu si wazima ila kwa upande wa kijana wako
Mambo si mambo kabisa"
“nani? Hafidhi au"....
Dennis akauliza hivyo,
“ndio ni Hafidhi binafsi amegeuka kuwa gaidi mpaka sasa kauwa polisi kumi na moja.
Dennis nakuomba please naitaji msaada wako uje kumzuia mwanafunzi
Wako asiendelee kufanya ugaidi"
“usijali baba yangu kesho
Nitakuja na vijana k**a watatu ni wakali zaidi yake tutamzuia tu,
Ondoa shaka kabisa kila kitu kitakwisha"
“nitashukuru sana kijana wangu
k**a kazi ikienda vizuri nitakupa cheo kikubwa sana"
Mzee J Ikram akakata simu
kabla hajaiweka mfukoni simu ikaita
akaipokea
“halloo Assalamu alaykum?
“waaleykum ssalamu
Ewe baba yangu"
Mzee J Ikram akashtuka na kuuliza
“wewe ni Hafidhi? please mwanangu rudi nyumbani uje kuniambia hao watu wamekufanyia kitu gani, tutawak**ata kwa mbinu za Kijeshi
kisha wajaze p**a kwa kisoda
au wale embe na kokwa lake,
Hafidhi mwanangu si unazifahamu vyema adhabu zetu ehee
basi njoo nyumbani Baba",,,,
yani aliongea huku kijasho kikimtoka kuonyesha ni jinsi gani anaitaji mwanae
arudi nyumbani.
Anampenda kuliko kitu chochote.
Mkewe akamnyang'anya simu
na kuongea yeye,
“Hafidhi baba uko wapi mwanangu?
Mama yako kila sekunde nalia nashindwa kula wala kulala"
“pole sana mama yangu"
Kisha akakata simu huku wakaishia kusema
halloo,,,,halloo,,,
Simu ishakatwa kibaya zaidi katumia simu ya mezani.
Ndani ya Yombo vituka tunamuona
Hafidhi akiwa anaongea na mama mmoja hivi.
“sawa kijana chumba umepata sema
ndani ya nyumba hii kuna mashart machache tu.
Utakiwi kutumia kilevi cha aina yeyote ile yani kuvuta bange sijui sigara"..
“usijali mama yangu yani hivyo vitu situmii kabisa"
“basi sawa subiri nikuandikie mkataba wako si umesema unahamia leo ehee?
“ndio nahamia leo maana ndio kwanza nimetoka kijijini nisije kulala stendi bure"
“inamaana hapa mjini huna ndugu
kabisa?"
“ndio sina ndugu
Nimekuja mjini kusaka maisha si naweza kupata kazi mama yangu ehee"..
“ndio kazi unaweza kupata ni uwezo wako tu na elimu yako, ehee unaitwa nani?"
Mwanaume akachekecha akili haraka akajibu
“naitwa Eddy Smith"
Basi yule mama akaandika
baadhi ya maneno kwenye karatasi ya mkataba kisha akamkabidhi
na funguo
“hizi ndio funguo za chumba chako
Kuhusu ratiba ya kufagia uwanja au kudeki choo utaenda kusoma pale chooni.
Kila chumba kina number imeandikwa kwenye mkataba"...
“sawa mama yangu nitafanya hivyo"
Hafidhi akaitikia na kuondoka zake,
Mwanaume akakodi pikipiki mpaka Ubungo kisha akaingia kwenye buss ya mwendo kasi
“kusema kweli dunia imekwisha zama zilizotabiriwa kuja ndio hizi yani kuna watu wanajiita manabii sijui mitume
Wakati mtume wa mwisho ameshakufa na hakuna tena mwinginewe mzuri k**a yeye"...
Ni mzee mmoja hivi alikuwa akiongea maneno hayo ndani ya buss
“wee mzee embu tunyamazie bwana naona unatupigia kelele tu",,,,
Ndani ya gari ikawa fujo mzee akatoka kwenye kuhubiri dini kaingia kwenye
Siasa
“unajuwa watanzaina walio wengi ni mambumbu inawezekana vipi kutaka kuwapa nchi wachaga,
Kwanza wachaga kwa hela wee wakipewa hii nchi hampati hata shilling kumi
Utasikia mama mia taka hogo"
Kuna kijana mmoja ambae ni mchaga akanyanyuka na kumkunja yule mzee
“wee mzee k**a ulitaka kuvunjiwa heshima
Mimi nakuvunjia
heshima kudadeki zako unaleta dharau na makabira ya watu sio?"
Hakika kijana yule aliongea povu likimtoka ikionyesha kachukia kuambiwa wao wachaga wanapenda pesa.
“tafadhali kijana niachie kabla sijaakurukia kichwa ohoo niachie nasema"..
Askari wa usalama aliyoko ndani ya gari hiyo akaja na kutuliza ghasia zile
Askari akamsihi yule kijana kwa kumwambia,
“wewe embu muachie kwanza huyu mzee"
Kijana hakukubari
“nitamuachaje bwana wakati kanitusi"
gari ikafika kituo kimoja ikasimama ikabidi wote wapigwe pingu na kushushwa safari kituoni wataenda kujibu mash*taka yao.
Ndani ya gari kukawa kimyaa mpaka inafika Kariakoo
Hafidhi akashuka na kuanza kukatiza mitaa
sijui kapajuwaje yani kila mtaa kila kichochoro akaingia,
Ndani ya gorofa moja hivi mwanaume akaingia na kupandisha ngazi
ndani ya chumba kimoja kulikuwa na watu wawili wakibishana
mmoja ni mzee wa makamo kwa kukadilia umri wake miaka k**a hamsini au stini.
mwingine ni binti mdogo tu
Mwenye umri wa miaka k**a ishillini
“kusema kweli binti yangu huyo kijana mimi simuhitaji kabisa na siku nikimuona amekanyaga hapa nitampasua kichwa"
“lakini baba yule ndio mpenzi wangu chaguo la moyo wangu"
“shatapu funga bakuri lako mwana izaya mkubwa wee mtoto huna hata haya, eti chaguo langu"
wakati wanaongea ghafla wakashtuka mlango ukipigwa teke akaingia kiumbe usoni amevaa maski nyeusi juu kavaa kofia aina ya pama,
“wee nani?
Yule mzee akaongea kwa kubabaika huku akifunua mto bila shaka alitaka kuitoa bastora, yake
Kiumbe chenyewe hakuwa mwingine ni
Hafidhi j Ikram kwa kasi ya kimbunga akamuwai yule mzee na kumuwekea kisu shingoni.
Binti yake akataka kukimbia kikarushwa kisu na kwenda kukita mlangoni.
“binti tulia tafadhali rudi hapa vinginevyo utamkosa Baba yako kuja hapa"....
Kwa sauti ya ukali
Mwanaume akaongea hivyo.
Yule binti akarudi kwa mwendo wa kutetemeka"
Hafidhi akaingiza mkono kwenye mto na kuichomoa bastora
“wee nani kwani?
Unataka nini kwangu?"
“usiwe na haraka ya kutaka kunijuwa mimi nani cha umuhimu naitaji zile pesa kiasi cha shilling million mia saba ziletwe hapa kisha utafahamu mimi ni nani"...
Hafidhi aliongea hivyo sijui hizo pesa kazijuwaje na huyu mzee kamfahamu vipi itakuwa barua ina siri nzito.
“pesa gani mbona mimi sina kitu"
Hafidhi akamshika yule binti na kufanya k**a anataka kulikata ziwa la binti yule
Kwa kisu.
“hapana kijana usifanye hivyo
huyo ni binti yangu ndio kila kitu kwangu please muache hizo
Pesa
nakupatia sasa hivi"....
Yule mzee akaongea hivyo huku akinyanyuka na kuingia kwenye chumba kimoja hivi na kutoka akiwa na begi,
“haya bibiye pokea hilo bag
Kisha fungua hiyo zipu nione"
Basi binti akafanya k**a alivyo ambiwa
Hafidhi baada kuridhika akalivaa lile bagi mgongoni na kuivua mask yake
Hakika mzee akash*tuka na kutamani hata kukimbia
“sikia nikwambie kitu mzee leo sijaja hapa kwa nia ya kuchukuwa roho yako.
Nimefata huu mzigo tu.
Sema una binti mzuri sana"
Hafidhi akamsogelea yule binti na kumpa mdomo
Ajabu binti akafumba macho na kuachia rips za midomo yake wazi.
Basi mwanaume akafanya aramba
Ahaaaaaa,,,ohooooooo binti akagugumia kwa raha
“binti unaitwa nani?
“naitwa Subira"
Mtoto kwa sauti tamu yenye kumtoa nyoka pangoni akajibu hivyo.
“basi chukuwa businesse card yangu hii nipigie baada nusu saa"
Subira akaipokea na kusema
“sawa mpenzi
Ving'ora vya magari ya polisi vikasikika kwa mbaali
Hafidhi kutizama hivi yule mzee hayupo kwenda kufungua mlango haufunguki umefungwa kwa nnje si kaleta mapenzi kwenye
kazi
Mwanaume akadata aisee
````````````````````````
https://m.facebook.com/storyza.k.fani
ENDELEA KULIKE HII PAGE KWA MASTORY ZAIDI GUSA HAYA MAANDISHI YA BLUE KISHA LIKE PAGE HIYO
Je nini kitaendelea?"
Je Hafidhi atatoka
Usikose kigongo hiki ngoma bado mbichi kabisa