Mjomba shop

Mjomba shop kifurushi karibu

08/05/2026

HADITHI: Mfalme na Mtihani wa Ladha
​Hapo zamani za kale, katikati ya pori nene la akiba, kulikuwa na bishano kubwa ambalo halijawahi kutokea. Punda Milia na Swala walikuwa wamesimama kwenye kilinge cha nyasi ndefu, kila mmoja akijigamba kuwa yeye ndiye mwenye nyama tamu kuliko mnyama yeyote mwituni.
​"Wewe Punda Milia, nyama yako ni ngumu k**a gome la mti!" alibeza Swala akiruka-ruka. "Nyama yangu mimi ni laini, ina ladha ya asali na harufu ya nyasi mbichi za asubuhi."
​Punda Milia alicheka kwa dharau, akapiga kwato zake chini na kusema, "Hujui usemalo! Nyama yangu ina mafuta ya wastani na nakshi ya mistari yangu inaingia hadi ndani ya mifupa. Mimi ndiye kitoweo cha thamani zaidi!"
​Bishano lilipamba moto hadi wakaamua kwenda kwa Mfalme Simba ili kutoa hukumu ya mwisho. Walimkuta Simba ameketi juu ya mwamba mrefu chini ya mbuyu, akijinyoosha huku jua la utosi likimulika manyoya yake ya dhahabu.
​"Ewe Mfalme wa Wafalme," walianza kwa unyenyekevu. "Tumekuja mbele yako utatue bishano letu. Nani kati yetu ana nyama tamu zaidi?"
​Mfalme Simba aliwatazama kwa macho yake makali yenye njaa iliyojificha. Alilamba midomo yake taratibu na kusema kwa sauti ya radi iliyotulia:
​"Hili ni suala zito. Na k**a mnavyojua, Mfalme hatoi hukumu kwa kusikia tu, bali kwa ushahidi wa vitendo. Ili nijue ukweli wa nani ana nyama tamu..."
​Simba alisimama, akawakaribia na kutoa amri iliyowafanya wanyama hao watetemeke magoti:
​"Amri yangu ni hii: Kila mmoja wenu akate kilo moja ya nyama kutoka kwenye paja lake, anipe hapa nionje sasa hivi. Atakayekuwa na nyama tamu zaidi, huyo ndiye nitakayemtangaza kuwa mshindi!"
​Porini kulizizima kwa ukimya. Swala na Punda Milia walitazamana, kila mmoja akijuta kwanini bishano hilo lilianza. Waligundua kuwa kutafuta sifa mbele ya adui, ni kualika mauti sebuleni kwako.
​Funzo la Hadithi:
Si kila bishano linahitaji mwamuzi, na si kila sifa inafaa kutangazwa; nyingine zinaweza kukuingiza kwenye matatizo makubwa.

15/10/2024
15/10/2024

Afcon Qualifications

1)- Sudan 🇸🇩 vs Ghana🇬🇭 2-0

2)- South Sudan 🇸🇸 vs Uganda 🇺🇬 1-2

3)- Chad 🇹🇩 vs Zambia 🇿🇲 0-1

4)- Lesotho 🇱🇸 vs Gabon 🇬🇦 0-2

5)- Malawi 🇲🇼 vs Senegal 🇸🇳 0-1

6)- Tanzania 🇹🇿 vs Dr Congo 🇨🇩 0-2

Habari zenu
05/05/2024

Habari zenu

11/02/2024

Premier League update:
Full-time
West Ham 0-6 Arsenal

11/02/2024

Kwa wapenzi wa tigo mambo ni huku
11/02/2024

Kwa wapenzi wa tigo mambo ni huku

*LEO TAR 02/10/2023 MWEZI WA ROSARI  TAKATIFU**MATENDO YA  FURAHA.* *(Jumatatu na Jumamosi)**Kwa jina la Baba na la Mwan...
02/10/2023

*LEO TAR 02/10/2023 MWEZI WA ROSARI TAKATIFU*

*MATENDO YA FURAHA.* *(Jumatatu na Jumamosi)*

*Kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu.Amina.*

*KANUNI YA IMANI.*

Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi,mwumba mbingu na dunia.Na kwa Yesu Kristu,mwanae wa pekee, Bwana wetu aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,akazaliwa na Bikira Maria akateswa kwa mamlaka ya ponsyo pilato,akasulibiwa,akafa,akazikwa,akashukia kuzimu,siku ya tatu akafufuka katika wafu,akapaa mbinguni amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi,toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,kanisa takatifu katoliki ushirika wa Watakatifu,maondoleo ya dhambi ,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.

*BABA YETU.*

Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe.Ufalune wako ufike.Utakalo lifanyike duniani k**a mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu k**a tunavyo wasamehe na sisi waliotukosea.Usisitutie katika kishawishi,lakini utuokoe maovuni.Amina.

*Naye atuzidishie Imani.*

Salamu Maria.....×1

*Naye atuongezee Matumaini.*

Salamu Maria.....×1

*Naye atuwashie Mapendo.*

Salamu Maria......×1

*ATUKUZWE BABA.*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. K**a mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milele,uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi huruma yako.

*TENDO LA KWANZA (1) KATIKA MATENDO YA FURAHA.*

*K.* Malaika anampasha habari Maria k**a atakuwa mama wa Mungu.
*W.* Tumuombe Mungu atujaliye Unyenyekevu.

*Baba yetu......×1*

*Salamu Maria.......×10*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. K**a mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milee,uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanaoitaji zaidi huruma yako.

*TENDO LA PILI (2) KATIKA MATENDO YA FURAHA.*

*K* Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti.
*W.* Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.

*Baba yetu.......×1*

*Salamu Maria.....× 10.*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu k**a mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milele.Uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi huruma yako.

*TENDO LA TATU (3) KATIKA MATENDO YA FURAHA*

*K.* Yesu anazaliwa Betlehemu
*W.* Tumwombe Mungu atujaliye Moyo wa ufukara.

*Baba yetu.....×1*

*Salamu Maria......× 10.*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.K**a mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele.Uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanahitaji zaidi huruma yako.

*TENDO LA NNE (4) KATIKA MATENDO YA FURAHA.*

*K.* Yesu anatolewa hekaluni
*W.* Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.

*Baba yetu.....×1*

*Salamu Maria......×10.*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.K**a mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milele.Uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi huruma yako.

*TENDO LA TANO (5) KATIKA MATENDO FURAHA.*

*K.* Maria anamkuta Yesu hekaluni.
*W.* Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

*Baba yetu.......×1*

*Salamu Maria........×10*

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.K**a mwanzo na sasa na siku zote na milele. *Amina.*

*K.* Ee Yesu mwema.
*W.* Utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milele.Uongoze Roho zote mbinguni hasa za wale wanaohitaji zaidi huruma yako.

*SALAMU MALKIA.*

Salamu Maria,Mama mwenye huruma uzima tulizo,matumaini yetu salamu.
Tunakusihi ugenini sisi wana Eva.Tukulilia tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi.Haya basi mwombezi wetu,utuangalie kwa macho yako yenye huruma.Na mwisho wa ugeni huu,utuonyeshe Yesu,mzao mbarikiwa wa tumbo lako.Ee mpole,ee mwema ,ee mpendelevu Bikra Maria.

*K.* Utuombee mzazi mtakatifu wa Mungu.
*W.* Tujaliwe ahadi za Kristu.

*TUOMBE.*

Ee Mungu, makimbilio na nguvu yetu,uwaangalie kwa wema watu wanaokulilia,na kwa maombezi ya Bikira Maria mtukufu asiye na kosa.Mzazi wa Mungu,na ya Mtakatifu Yosefu,mchumba wake na ya Watakatifu Petro na Paulo mitume wako,na ya Watakatifu wote.Usikilize kwa huruma na wema sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na kwa uhuru na utukufu wa kanisa,mama mtakatifu.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.

*LITANIA YA BIKIRA MARIA.*

*K.* Bwana utuhurumie... *W.* Bwana utuhurumie.

K.Kristu utuhurumie...W.Kristu utuhurumie.

K.Bwana utuhurumie...W.Bwana utuhurumie.

K.Kristu utusikie....W.Kristu utusikilize.

K.Baba wa mbinguni,Mungu..W.Utuhurumie.

K.Mwana mkombozi wa dunia Mungu...W.Utuhurumie.

K.Roho Mtakatifu, Mungu...W.Utuhurumie.

K.Utatu Mtakatifu,Mungu mmoja...W.Utuhurumie.
K.Maria Mtakatifu...W.Utuombeee.
Mzazi mtakatifu wa Mungu...utuombee.
Bikira mtakatifu mkuu wa mabikira...utuombee.
Mama wa Kristu..utuombee.
Mama wa neema ya Mungu...utuombee.
Mama mtakatifu sana...utuombee.
Mama mwenye usafi wa moyo..utuombee.
Mama usiye na doa..utuombee.
Mama usiye na dhambi...utuombee.
Mama mpendelevu...utuombee.
Mama msitaajabivu...utuombee.
Mama wa shauri jema...utuombee.
Mama wa mwumba...utuombee.
Mama wa mkombozi...utuombee.
Bikira mwenye utaratibu...utuombee.
Bikira mwenye heshima ...utuimbee.
Bikira mwenye sifa...utuombee.
Bikira mwenye enzi...utuombee.
Bikira mwenye huruma...utuombee.
Bikira amini...utuombee.
Kioo cha haki...utuomber.
Kikao cha hekima...utuombee.
Sababu ya furaha yetu...utuombee.
Chombo cha neema...utuombee.
Chombo cha heshima...utuombee.
Chombo bora cha ibada...utuombee.
Waridi lenye fumbo..utuombee.
Mnara wa Daudi..utuombee.
Mnara wa pembe...utuombee.
Nyumba ya dhahabu..utuombee.
Sanduku la Agano...utuombee.
Mlango wa mbingu...utuombee.
Nyota ya asubuhi...utuombee.
Afya ya wagonjwa...utuombee.
Makimbilio ya wakosefu...utuombee.
Mfariji wa wenye uchungu...utuombee.
Msaa wa wakristu...utuombee.
Malkia wa malaika..utuombee.
Malkia wa mababu...utuombee.
Malikia wa manabii...utuombee.
Malkia wa mitume...utuombee.
Malkia wa mashaidi...utuombee.
Malkia wa waungama..utuombee.
Malkia wa mabikira...utuombee.
Malkia wa watakatifu wote...utuombee.
Malikia uliye umbwa pasipo dhambi ya asili...utuombee.
Malkia uliyepalizwa mbinguni...utuombee.
Malkia wa Rozari takatifu...utuombee.
Malkia wa amani..utuombee.

*K.* Mwana kondoo wa Mungu,uondoaye dhambi za Ulimwengu.
*W.* Utusamehe ee Bwana.

*K.* Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za Ulimwengu.
*W.* Utusikilize ee Bwana.

*K.* Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za Ulimwengu.
*W.* Utuhurumie.

*K.* Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
*W*. Tujaliwe ahadi za Kristu.

*TUOMBE.* Ee Mungu,utujalie sisi watumishi wako afya ya mwili na roho siku zote.Tuopolewe na mashaka ya sasa kwa maombezi ya Maria mtakatifu,Bikira daima ili tupate furaha ya milee.
Tunaomba hayo kwa kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.

*KUMBUKA.*
Kumbuka,ee Bikira mpore haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako,aliyeomba msaada na maombezi yako.
Kwa matumaini hayo nakukimbilia ee,Mama mkuu mabikira.Ninakuja kwako nasimama mbele yako,nikilalamika mimi mkosefu,ewe mama wa Neno wa Mungu.Naomba usikatae maneno yangu bali uyasikilize.Amina.

*TUNAUKIMBILIA.*
Tunaukimbilia ulinzi wako,mzazi Mtakatifu wa Mungu,usitunyime tukiomba katika shida zetu,utukoe siku zote kila tuingiapo hatarini ewe Bikira mtukufu na mwenye baraka. *Amina.*

*Kwa jina la Baba na la mwana na Roho Mtakatifu .Amina.*

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255676951027

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mjomba shop posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mjomba shop:

Share