11/07/2025
MTAMANI TV
NDWATI, KIBAHA VIJIJINI – PWANI
Usiku wa tarehe 09/07/2025, ulitikiswa na tukio la wizi uliofanywa kwenye duka la mwanakijiji cha Ndwati (Jina tunalo) na kupelekea wananchi wenye hasira kali kumdhibiti mmoja wao na alipokuwa mkaidi wakampiga na kupoteza maisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndwati, Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kwa maelezo ya viongozi hao walisema, mwenye Duka anaishi karibu na Duka lake, usiku huo alisikia vishindo vilivyofanya aamke na kwenda Dukani na kukuta watu wawili wanatoka na kufanikiwa kukimbia.
Mmoja alichelewa kutoka na alipotoka alikuta baadhi ya wanakijiji walioshtushwa na mayowe ya mwenye duka kuwa wezi wanaiba kwenye duka lake.
Kitendo hicho kikapelekea kumkimbiza mwizi aliyechelewa kutoka dukani na kufanikiwa kumdhibiti baada ya kumkimbiza k**a urefu wa mita mia moja kutoka dukani.
Baada ya taratibu zote kufanywa na viongozi wa Kijiji cha Ndwati, askari walifika eneo la tukio na Daktari kwa lengo la kuthibitisha k**a kipigo alichopata mwizi kimesababisha afariki au la, na taratibu zingine kufanywa.
Ilipothibitika kuwa mwizi amefariki kutokana na kipigo, na kukutwa na baadhi ya vitambulisho vilivyokuwa na taarifa zake, viongozi wa Kijiji walifanya mawasiliano na kugundua kuwa mwizi alikuwa mwenyeji wa Ngerengere, Mkoa wa Morogoro.
Mawasiliano yalifanyika na ndugu wa marehemu, ndugu walifika eneo la tukio na kukabidhiwa mwili kwa ajili ya mazishi baada ya kupewa taarifa ya tukio.
Hata hivyo, ndugu walielezwa kuwa, endapo watakuwa na jambo lolote linalohusiana na tukio hilo, wafike kituo cha Polisi Kibaha.
MTAMANI TV