Mzunguko Online

Mzunguko Online Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mzunguko Online, Photography Videography, Mkwajuni, CCM Makongo Juu, Dar es Salaam.

Serikali imethibitisha kuwa bado kuna mahitaji ya uanzishwaji wa vyuo vya uuguzi na uganga katika maeneo mbalimbali ya n...
29/05/2025

Serikali imethibitisha kuwa bado kuna mahitaji ya uanzishwaji wa vyuo vya uuguzi na uganga katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwa ni pamoja na wilaya ya Ukerewe ambapo kwa sasa juhudi zimeelekezwa kwenye ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa katika wilaya hiyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe, Mhe. Joseph Michael Mkundi, leo Mei 29, 2025 Bungeni Jijini Dodoma, alilyetaka kufahamu ni lini Serikali itajenga tawi la Chuo cha Uuguzi na Uganga Ukerewe, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa Serikali itaendelea kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini k**a kuna uhitaji wa kuanzisha Chuo cha Uuguzi katika eneo hilo, mara baada ya kukamilika kwa hospitali hiyo.

“Ni kweli bado kuna mahitaji ya vyuo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ila kwa sasa Serikali inajenga hospitali yenye hadhi ya Rufaa ya Mkoa katika wilaya ya Ukerewe. Sambamba na ujenzi huo, Serikali itaendelea kufanya upembuzi yakinifu kuona k**a eneo hilo litahitaji kuwa na Chuo cha Uuguzi,” amesema Dkt. Mollel.

Hapo jana, mataifa 12 ikiwemo Rwanda yamelaani hatua ya M23 kujenga utawala mbadala mashariki mwa DRC .M23 wanatuhumiwa ...
29/05/2025

Hapo jana, mataifa 12 ikiwemo Rwanda yamelaani hatua ya M23 kujenga utawala mbadala mashariki mwa DRC .

M23 wanatuhumiwa kwa kukiuka haki za binadamu na kudhibiti maeneo makubwa tangu Januari.

Hii imeubua mshangao kwa watu wengi kwani Rwanda, ambayo kwa muda mrefu imehusishwa na kuwaunga mkono waasi hao, sasa inaanza kuhoji msaada wake kwao.

Racquel “Kelly” Smith (35) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumteka na kumuuza binti yake kwa mganga, akisai...
29/05/2025

Racquel “Kelly” Smith (35) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumteka na kumuuza binti yake kwa mganga, akisaidiana na washirika wake wawili.

Mganga huyo akihojiwa, alidai kuvutiwa na macho ya mtoto na rangi ya ngozi yake. Hii ni sababu ya kikatili sana iliyosababisha mtoto huyo kupoteza maisha na ndoto zake.

Baada ya kuongoza kampeni ya kupunguza matumizi serikalini kupitia Idara ya Ufanisi Serikalini (DOGE), bilionea Elon Mus...
29/05/2025

Baada ya kuongoza kampeni ya kupunguza matumizi serikalini kupitia Idara ya Ufanisi Serikalini (DOGE), bilionea Elon Musk ameandika ujumbe wa kuagana kwenye X:

“Ninamshukuru Rais Trump kwa kunipa fursa ya kutumikia taifa kupitia DOGE.”

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kauli kali dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, kufuatia mashambulio ya anga yali...
26/05/2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kauli kali dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, kufuatia mashambulio ya anga yaliyofanywa na Moscow kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drone) dhidi ya miji mbalimbali ya Ukraine, kuamkia siku ya Jumapili.

Trump amesema kitendo cha Urusi kuendeleza mashambulio hayo ni cha kihuni na kisicho na heshima, hasa ikizingatiwa kwamba Moscow na Kyiv hivi karibuni walikamilisha ubadilishanaji wa wafungwa, hatua iliyotafsiriwa na wengi kuwa mwanzo wa kupunguza mvutano.

“Putin amevunja matumaini ya diplomasia ya kweli. Dunia inatazama, na ni wazi kuwa Urusi haijachoka na ghasia. Ni wakati wa mataifa yote kupaza sauti kwa ajili ya Ukraine,” alisema Trump mbele ya waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa duru za kijeshi, mashambulio hayo yamelenga miundombinu ya raia katika miji ya Kyiv, Dnipro na Kharkiv, yakisababisha uharibifu mkubwa na majeruhi, licha ya juhudi za Ukraine kuzizuia kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa anga.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea na mikakati ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania n...
26/05/2025

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea na mikakati ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Japan ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika mataifa hayo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza tija kubwa kwenye masuala ya biashara na uwekezaji.

Amesema hayo leo (Jumatatu, Mei 26, 2025) alipofungua kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ...
26/05/2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuruhusu kuendelea kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa hoteli ya nyota tano katika eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Mradi huo unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unalenga kubadilisha mandhari ya Jiji la Mwanza na kulifanya kuwa kitovu cha utalii, mikutano ya kimataifa na biashara katika Kanda ya Ziwa.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa maono yake ya kimkakati na kwa kuunga mkono maendeleo ya Mwanza. Hoteli hii itakuwa na mchango mkubwa kwa ajira, mapato ya serikali na ukuzaji wa sekta ya utalii,” alisema RC Mtanda.

Hoteli hiyo ya kisasa itakuwa na miundombinu ya hali ya juu, ikiwemo vyumba vya wageni wa kimataifa, kumbi za mikutano, maeneo ya burudani, na huduma bora za malazi, hivyo kuimarisha hadhi ya Mwanza kimataifa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya ...
26/05/2025

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa chama kujadili masuala muhimu ya kisera, maendeleo ya chama na mustakabali wa kisiasa wa Taifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kikao hiki ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha CCM inaendelea kujiimarisha kitaasisi, kisiasa na kimkakati, huku ikichambua kwa kina masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yanayoikabili nchi kwa sasa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais- TAMISEMI imefanya kikao maalum cha ...
26/05/2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais- TAMISEMI imefanya kikao maalum cha mashauriano ya kiufundi na wadau wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Shirika la GFF la Marekani, JICA kutoka Serikali ya watu wa Japan na KFW ya Ujerumani, ikiwa ni hatua za awali za maandalizi ya utekelezaji wa Mpango Endelevu wa Mageuzi na Ubunifu katika Sekta ya Afya (SHIFT).

Kikao hicho kilichofanyika kwa siku tano, Jijini Dar es Salaam na kuhitimishwa Mei 23, 2025, kililenga kubadilishana uzoefu wa kitaalam katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na mipango mahususi ya kuharakisha utekelezaji wa afua za uboreshaji wa utoaji wa huduma za afya hapa nchini.

Akifungua rasmi kikao hicho, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Bw. Amoury Amoury, amesisitiza dhamira ya kikao hicho maalumu katika kuweka misingi imara ya utekelezaji wa Mpango wa SHIFT kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, ikiwa ni pamoja na: kuimarisha huduma za dharura na magonjwa ya mlipuko, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote (UHI), kuboresha mifumo ya afya ya jamii na huduma za magonjwa yasiyoambukiza (NCDs), miundombinu ya maabara, na mifumo ya kidijitali ya afya.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, ametoa maelekezo kwa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kuhakikisha abi...
26/05/2025

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, ametoa maelekezo kwa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kuhakikisha abiria wanaokumbwa na ucheleweshaji (delays) au kughairiwa kwa safari (cancellations) wanapatiwa huduma za msingi bila ubaguzi.

“Nawaelekeza ATCL kuhakikisha kwamba pale tunapofanya cancellation au delays, wahakikishe kwamba abiria anapewa huduma za msingi, ikiwa ni pamoja na chakula, kutokana na usumbufu ambao kimsingi anakuwa anaupata,” amesema Naibu Waziri Kihenzile.

Ameeleza kuwa ni haki ya kila abiria kupata huduma ya heshima na stahiki kulingana na hali anayopitia, na kwamba hatua hiyo inalenga kuimarisha huduma kwa wateja na kuijenga imani ya umma kwa mashirika ya usafiri wa anga nchini.

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ametoa wito mzito kwa viongozi wa Afrika kuwa wakweli, waadilifu na waaminif...
24/05/2025

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ametoa wito mzito kwa viongozi wa Afrika kuwa wakweli, waadilifu na waaminifu katika kulinda na kutetea maslahi ya bara lao, ili kuweka msingi imara wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu wa Afrika.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi na wanazuoni kuhusu mustakabali wa Afrika, Mbeki amesema kuwa ili bara hilo lipige hatua, lina wajibu wa kujenga viongozi wanaosimama kwa misingi ya uwajibikaji, uongozi wa kweli na weledi.

“Hatuwezi kufanikisha ndoto ya Afrika yenye maendeleo k**a tunaendelea kuwa na viongozi wanaotanguliza maslahi binafsi mbele ya maslahi ya wananchi,” amesema Mbeki.

Kwa mujibu wake, mapambano dhidi ya rushwa, udikteta wa kisiasa na utawala wa hovyo ndio msingi wa kuimarisha ustawi wa bara hilo lenye rasilimali nyingi lakini bado linakabiliwa na changamoto kubwa za maendeleo.

Mbeki pia amesisitiza umuhimu wa umoja wa Afrika, utawala bora, na uwekezaji kwenye elimu, afya na miundombinu ili kukuza uchumi wa bara hilo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Mahak**a nchini Uganda imekataa ombi la dhamana lililowasilishwa kwa niaba ya Dkt. Kizza Besigye, kiongozi wa muda mrefu...
24/05/2025

Mahak**a nchini Uganda imekataa ombi la dhamana lililowasilishwa kwa niaba ya Dkt. Kizza Besigye, kiongozi wa muda mrefu wa upinzani na mpinzani wa karibu wa Rais Yoweri Museveni, licha ya kuwa ameshikiliwa kwa zaidi ya miezi sita bila kufikishwa mahak**ani.

Dkt. Besigye (69), ambaye hapo awali aliwahi kuwa daktari binafsi wa Rais Museveni kabla ya kugeuka kuwa mpinzani wake mkubwa, anakabiliwa na shtaka la uhaini, shtaka zito linaloweza kupelekea adhabu ya kifo endapo atapatikana na hatia.

Waendesha mashtaka walidai kuwa Besigye bado ni tishio kwa usalama wa taifa na kwamba kumuachia kwa dhamana kunaweza kusababisha machafuko ya kisiasa. Wakili wa Besigye amesema wateja wake wanasikitishwa na uamuzi huo, wakilitaja kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria ya haki ya kusikilizwa ndani ya muda unaokubalika kisheria.

“Huu ni ukiukaji mkubwa wa haki za msingi za raia. Dkt. Besigye ana haki ya kujitetea akiwa huru, hasa kwa kuwa hajawahi kufikishwa rasmi mahak**ani kwa zaidi ya miezi sita,” amesema mmoja wa mawakili wake.

Address

Mkwajuni, CCM Makongo Juu
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mzunguko Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mzunguko Online:

Share