22/03/2026
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya Kilimanjaro International Marathon 2027.
Makonda amesema hayo leo, Machi 22, 2026 wakati akizindua mbio hizo, jijini Arusha na kueleza kuwa zawadi kwa washindi itakuwa zaidi ya shilingi milioni 100.