Free Church of Life-FCOL Kanisa Huru la Maisha

Free Church of Life-FCOL Kanisa Huru la Maisha FREE CHURCH-FC (KANISA HURU). FOUND OLJORO JKT NEARBY ARUSHA SCIENCE, ARUSHA-TANZANIA: The Church affirms the authority & inerrancy of the Bible.

The Trinity atonement through the sacrifice of Jesus Christ.

12/04/2026

Mwanzo 1:2. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Tunajifunza uwepo wa mpangilio na mgawanyiko wa vitu katika UUMBAJI, kwanza tuna NCHI, pili MAJI, tatu GIZA.

Katika mpangilio huu Kuna vitu vitatu Mungu alivipanga kwa mfuatano vikiwa vinaelea katika MBINGU (Anga) ambavyo ni NCHI, MAJI na GIZA.

Kwa kuwa Giza lilikuwa juu ya Uso wa vilindi vya maji, Roho ya Mungu (nafsi) ilitulia juu ya uso wa maji ili kuepusha madhara ya giza katika utendaji wake wa kazi kwa kuwa Roho ya Mungu ndio alikuwa ameandaliwa kwa ajiri ya kutoka amri juu ya vitu vyote vitatu ili kuwepo na uwiano mzuri wa kimpangilio na tabia za kimazingira.

NCHI (sayari) zote ziliwekwa katika mfumo wa mfuatano na vitu viwili yaani (Maji na giza), kwahio matukio yanayotokea katika NCHI moja ni sawa kwa NCHI zote isipokuwa tofauti yake ni masaa, siku, mwaka au (muda).

Nuru (Mchana) huifanya Kila NCHI ipate mwanga, joto na tabia za nchi zinazotokana na Nuru asili ambayo ni Jua.

Giza (Usiku) huifanya Kila NCHI ipate Giza ili kupoza joto la Nuru na kufanya tabia ya NCHI husika kutokea au kubalansi kwa usitawi wa viumbe vyake.

Hivyo Kila NCHI hupata Nuru na giza kwa muda tofauti kulingana na mahali au umbali ilipo kutoka chanzo Cha Nuru yaani Jua na mara baada ya Nuru kutoweka Giza huingia mahali Hapo.

Maji husafiri katika Hali mbalimbali kuifikia Kila NCHI, Hali hizo ni kimiminika, yabisi mara chache na mvuke kwa wingi.

Hivyo maji nayo yako katika mzunguko wa kwenda katika NCHI na kurudi katika MBINGU (Anga).

Kwa kukamilisha mifumo hiyo yote ya kutegemeana katika NCHI Roho wa Mungu (nafsi) alibaki juu ya uso wa vilindi vya maji juu yake kukiwa na GIZA anayemruhusu aifikiye Kila NCHI kwa wakati na kuondoka.

Ndipo Roho wa Mungu aliteua baadhi ya NCHI akazipa nafsi kupitia maumbo na matabaka mbalimbali k**a vile binadamu, wanyama, miti na viumbe hai vingine vyote.

Moja ya NCHI iliyopewa nafsi nyingi katika maumbo mbalimbali ni Dunia, NCHI zingine zilipewa nafsi chache na zingine zinautupu zikiwa na nafsi moja kuu peke yake iwezayo kuishi Kila mahali (Roho wa Mungu).

Watu wa Mungu Kila mmoja wetu ni muhimu kujijali na kuyatunza maumbile ya nafsi na NCHI ya mahali alipo ili kuendeleza usitawi wetu wa asili.

Neno NCHI kwa tafsiri ya Roho ya Mungu ni Sayari au umbo lolote lililoko katika MBINGU na lenye uwezo au lisilo na uwezo wa kuizunguka Nuru.

Hivyo NCHI sio hivi vipande vya NCHI moja vinavyogombaniwa na wanadamu hii leo.

NCHI (Sayari) Dunia ni NCHI moja miongoni mwa NCHI nyingi zinazoelea katika MBINGU (Anga).

Inua Huduma kwa Kuisapoti kupitia Akaunti namba 0152418952200 CRDB Benki au Lipa namba ya Vodacom 57241899 Jina Rev.Tr.Pius Kusekwa Elias.

Mawasiliano: +255 785 241 032/+255 755 646 810, Rev.Tr.Pius Kusekwa Elias.

Kanisa la Free Church of Life -FCOL Mji Mwema Laroi Arusha TANZANIA.

Watu wa Mungu jiandaeni kwa ajili ya somo linalofuata.Somo litatoka katika kitabu Cha Mwanzo 1:2 likiwa ni mwendelezo wa...
12/04/2026

Watu wa Mungu jiandaeni kwa ajili ya somo linalofuata.

Somo litatoka katika kitabu Cha Mwanzo 1:2 likiwa ni mwendelezo wa UUMBAJI na jinsi maisha yalivyoanza katika nchi mbalimbali (Neno nchi) limesimama badala ya Sayari na maumbo mbalimbali ndani ya MBINGU.

Mwanzo 1:2. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, Tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Nitatoa ufafanuzi zaidi ili Kila mfuasi wetu apate kuelewa juu ya kifungu hiki vyema.

Inua Huduma kwa Kuisapoti kupitia Akaunti namba 0152418952200 CRDB Benki au Lipa namba ya Voda 57241899 Jina Rev.Tr.Pius Kusekwa Elias

Kanisa la Free Church of Life -FCOL Mji Mwema Laroi Arusha.

UUMBAJI.UUMBAJI ni kitendo Cha kutengeneza kitu kipya au kuendeleza maarifa ya kitu kilichokuwepo awali.Kitabu Cha Mwanz...
12/04/2026

UUMBAJI.
UUMBAJI ni kitendo Cha kutengeneza kitu kipya au kuendeleza maarifa ya kitu kilichokuwepo awali.

Kitabu Cha Mwanzo 1:1 Kinatueleza namba na jinsi Mungu alivyoanza kufanya kazi ya UUMBAJI.

Mwanzo 1:1 Hapo Mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Kifungu hiki Cha maneno ya Mungu katika UUMBAJI Kinatueleza kuwa UUMBAJI wa kwanza kabisa ni UUMBAJI wa mbingu na nchi.

MBINGU ni Nini katika kitabu Cha Mwanzo.

MBINGU ni nafasi au uwazi kutoka mahali mahali palipo na ardhi ya Kila Sayari, uwazi huu hauna ukomo na huzitenganisha sayari moja na nyingine.

Kila sayari inambingu (anga) linaloizunguka, anga la Kila sayari hutengeneza Hali ya hewa ya mahali pale kulingana na mahali sayari hiyo ilipo.

NCHI ni mjumuiko wa maumbo yote makubwa na madogo yanayopatikana katika uwazi ( MBINGU) na Kila umbo ni nchi kutokana na aina ya udongo, majabali na mjumuiko wa namna mahali pale palivyojitengeneza na kubadilika kulingana na tabia ya nchi.

Umri wa MBINGU na NCHI ni sawa kwa kuwa ziliumbwa kwa pamoja na ndio Mwanzo wa UUMBAJI.

Maisha ya viumbe hai wengine katika sayari na maumbo yaliyomo katika MBINGU hutegemeana na tabia ya nchi ya mahali Umbo au sayari ilipo.

Kumbe kinaweza kuishi kwa muda mfupi zaidi au mrefu zaidi kulingana na tabia ya nchi ya mahali kilipo kiumbe hicho.

Viumbe vingi na kwa asilimia kubwa viliwekwa Kuishi juu ya uso wa umbo (Sayari) iitwayo Dunia maana ndipo palipo na tabia ya nchi rafiki kwa maisha ya viumbe hivi akiwemo binadamu.

Pamoja na viumbe hivi kuishi katika uso na ardhi ya Dunia bado zimetengwa katika mazingira yanayovisaidia Kila kimoja, ndio maana vipo viumbe Viko mahali Fulani kwenye uso wa Dunia lakini havipo mahali Fulani kwenye uso wa Dunia hio hio maana siyo mahali pake kuishi.

Hivyo kuhama au kuhamishwa kwa viumbe kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine kinaweza kuwa na mazara chanya au hasi.

Kuishi kwa viumbe kwenye mazingira mapya kinaweza kuongeza siku za uhai au kupungu siku hizo zaidi.

Kwa mfano kiumbe kinachoishi katika Uso wa Dunia kwa siku thelathini kinaweza kuishi katika Uso wa umbo la mwezi kwa siku 15 au chini ya Hapo.

Lakini kiumbe hicho kikiishi kwenye uso wa mwezi kwa siku zaidi ya thelathini kutakuwa na matokeo chanya ya maisha ya aina ya viumbe hizo mwezini ila kikiishi chini ya siku thelathini katika Uso wa mwezi kutakuwa na matokeo hasi ya viumbe hivyo kuishi katika uso wa mwezi.

Kwahio matokeo ya maisha katika Uso wa maumbo mbalimbali ni matokeo ya mazingira, uzalishaji wa mahitaji ya Kila siku, na uzalianaji wake kiurahisi.

Inua Huduma kwa Kuisapoti kupitia Akaunti namba 0152418952200 CRDB Benki au Lipa namba ya Voda 57241899 Jina Rev.Tr. Pius Kusekwa Elias.

Tufuatilie na karibu katika Kurasa zetu za VOICE OF TANZANIA - VOT na kanisa la Free Church of Life_FCOL Mji Mwema Laroi Arusha au piga simu namba 0785 241 032/ +255 755 646 810 Rev.Tr. Pius Kusekwa Elias.

.Tr.Pius Kusekwa Elias

Inua Huduma: Changia Uenezaji wa injili Duniani kwa namba +255 755 646 810/+255 785 241 032, Jina Rev.Tr Pius Kusekwa El...
11/04/2026

Inua Huduma:
Changia Uenezaji wa injili Duniani kwa namba +255 755 646 810/+255 785 241 032, Jina Rev.Tr Pius Kusekwa Elias

Inua Huduma.Changia Uenezaji wa injili Duniani kwa namba 0785 241 032/ 0755 646 810 au Lipa namba 57241899 Jina Rev.Tr. ...
11/04/2026

Inua Huduma.
Changia Uenezaji wa injili Duniani kwa namba 0785 241 032/ 0755 646 810 au Lipa namba 57241899 Jina Rev.Tr. Pius Kusekwa Elias.

09/04/2026

God bless all nations world wide

FREE CHURCH-FC (KANISA HURU). FOUND OLJORO JKT NEARBY ARUSHA SCIENCE, ARUSHA-TANZANIA: The Church affirms the authority ...
21/02/2022

FREE CHURCH-FC (KANISA HURU). FOUND OLJORO JKT NEARBY ARUSHA SCIENCE, ARUSHA-TANZANIA: The Church affirms the authority & inerrancy of the Bible. The Trinity atonement through the sacrifice of Jesus Christ.

Address

Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Free Church of Life-FCOL Kanisa Huru la Maisha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Free Church of Life-FCOL Kanisa Huru la Maisha:

Share

Category