09/10/2026
Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, amewarai viongozi wenzake wa upinzani dhidi ya kupinga kila kitu kinachofanywa na Rais William Ruto. Kalonzo anasisitiza kuwa upinzani unapaswa kuwa wa haki na wenye uwajibikaji, ukikosoa pale ambapo serikali imekosea na kupongeza pale ambapo kuna miradi na hatua za maendeleo zinazostahili kutambuliwa. Amesema kuwa miradi k**a kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote na barabara ya Rironi–Mau Summit inafaa kutazamwa kwa mtazamo wa maendeleo badala ya siasa za kupinga kila jambo.