Epl,La Liga,Serie A, Bundesliga-Kiswahili

Epl,La Liga,Serie A, Bundesliga-Kiswahili Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Epl,La Liga,Serie A, Bundesliga-Kiswahili, Dar es Salaam.

Ukurasa huu ni mahsusi kwa ajili ya kukuletea habari zinazohusu vilabu vya ligi kuu nne bora za soka barani Ulaya,ambazo ni Ligi kuu ya Uingereza(EPL),Ligi Kuu ya Uhispania(La liga),Ligi kuu ya Ujerumani(Bundesliga) na Ligi kuu ya Italia(Serie A).

09/11/2025

Matokeo ya leo EPL Crystal Palace 0-0 Brighton Aston Villa 4-0 AFC Bournemouth , E Buendia (28), A Onana (40), R Barkley (77), ...

09/11/2025

Ligi kuu ya Uingereza yazidi kushika kasi wikiendi ya 10 tangu ligi kuu ya UING EREZA ianze msimu huu imeshuhudia kandanda safi na yenye k...

  Sare ya kwanza ya michuano ya mataifa ya Ulaya 2024 imepatikana mara baada ya Denmark kufungana bao 1-1 na Slovenia.Ba...
16/06/2024


Sare ya kwanza ya michuano ya mataifa ya Ulaya 2024 imepatikana mara baada ya Denmark kufungana bao 1-1 na Slovenia.
Bao la uongozi la Denmark lilifungwa na Christian Eriksen dakika ya 17. Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika. Kipindi cha pili Denmark ilianza kwa kasi kwa lengo la kuongeza bao jingine bila ya mafanikio.
Kocha Matjaž Kek wa Slovenia akafanya mabadiliko kwa kuwatoa Petar Stojanović(67'), Jan Mlakar(75') na Timi Max Elšnik(76'), na nafasi zao kuchukuliwa na Benjamin Verbič, Žan Celar na Jon Gorenc Stanković. Mabadiliko hayo yaliifanya Slovenia kutawala mchezo na kusawazisha kwa shuti kali la beki Erik Janža dakika ya 77.
Siku ya Alhamisi Denmark watakutana na Serbia huku Slovenia wakikutana na England katika muendelezo wa mechi za kundi C.

  Uholanzi imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Poland huko mjini Hamburg.Bao la dakika ya 16 la Adam B...
16/06/2024


Uholanzi imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Poland huko mjini Hamburg.
Bao la dakika ya 16 la Adam Buksa liliipa uongozi wa muda mfupi timu ya taifa ya Poland,kabla ya mshambuliaji hatari Cody Gakpo kuwasawazishia Uholanzi dakika ya 29.
Baada ya bao hilo la kusawazisha,Uholanzi walipambana kupata bao la kuongoza bila mafanikio mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Dakika ya 81 kocha Ronald Koeman akaamua kufanya mabadiliko kwa kumtoa mshambuliaji Memphis Depay na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Wout Weghorst. Weghorst alifunga bao la ushindi kwa Uholanzi dakika mbili baadaye.

 Kiungo wa timu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Uruguay Rodrigo Bentancur amemuomba radhi mchezaji mwenzake Son...
15/06/2024


Kiungo wa timu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Uruguay Rodrigo Bentancur amemuomba radhi mchezaji mwenzake Son Heung-min kutokana na maneno ya kibaguzi aliyoyasema hivi karibuni.
Mchezaji huyo alisikika katika video akisema "Raia wote wa Korea Kusini wanafanana".

Katika video fupi iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kupitia kipindi cha Por la Camiseta cha Televisheni huko Uruguay,mtangazaji Rafa Cotelo alionekana akimuomba jezi ya Tottenham mchezaji huyo, Rodrigo akajibu" unataka ya Son!?,inaweza ikawa ya binamu yake Son kwa sababu wanafanana!. Bentancur aliomba radhi baada ya maneno yake kukosolewa.
"Kaka yangu Son,naomba unisamehe kwa utani wangu mbaya",aliandika Bentancur kwenye mtandao wa Instagram.

 Golikipa wa klabu ya Millwall na timu ya taifa ya Montenegro Matija Sarkič amefariki asubuhi ya leo huko mjini Budva-Mo...
15/06/2024


Golikipa wa klabu ya Millwall na timu ya taifa ya Montenegro Matija Sarkič amefariki asubuhi ya leo huko mjini Budva-Montenegro akiwa na umri wa miaka 26. Inasemekana kwamba alianguka ghafla akiwa nyumbani kabla ya kupoteza maisha.
Mchezaji huyo alisajiliwa na Millwall mwaka jana na kucheza mechi 33 katika msimu wa 2023-2024. Pia alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ubelgiji wiki iliyopita.

 Timu ya taifa ya Ujerumani iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Scotland kwenye mechi ya ufunguzi hapo jana mjini ...
15/06/2024


Timu ya taifa ya Ujerumani iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Scotland kwenye mechi ya ufunguzi hapo jana mjini Munich.
Bao la kwanza la Ujerumani lilifungwa na mshambuliaji hatari wa Bayer 04 Leverkusen Florian Wirtz ndani ya dakika 10 za mchezo. Mabao mengine ya Ujerumani yalifungwa na Jamal Musiala(19'),Kai Havertz( pen 45'),Niclas Füllkrug(64'),Emre Çan(93'), na bao la kujifunga la mlinzi Antonio Rüdiger lililofungwa dakika ya 87 liliwafuta machozi vijana kutoka Scotland.

Scotland 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 Nahodha wa timu ya taifa ya Scotland, Andy Robertson,amesema timu yao ya taifa kwa sasa haitataka kupat...
14/06/2024

Scotland 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿

Nahodha wa timu ya taifa ya Scotland, Andy Robertson,amesema timu yao ya taifa kwa sasa haitataka kupata majuto ya aina yoyote,hasa pale watakapokutana na miamba wa timu ya taifa ya Ujerumani katika mechi ya ufunguzi wa Euro 2024 usiku wa leo.
Nahodha huyo amesema uwezekano wa wao kuwa timu ya kwanza katika historia ya soka la Scotland kuingia hatua za mtoano za michuano hiyo,inawapa hamasa kubwa.Mara ya mwisho kwa timu hiyo inayonolewa na Steve Clarke kufuzu michuano hiyo ilikuwa ni mwaka 2021,ambapo walimaliza mechi zao na alama moja na bao moja pekee.

  inahitaji walau £80M(Sh.264 bilioni) ili kumwachia mlinzi wao wa katiJarrad Branthwaite. Timu za Manchester United ,Ch...
14/06/2024

inahitaji walau £80M(Sh.264 bilioni) ili kumwachia mlinzi wao wa kati
Jarrad Branthwaite. Timu za Manchester United ,Chelsea na Newcastle zinamuhitaji mchezaji huyo raia wa Uingereza.

  imemsajili winga mashuhuri Guilherme mwenye umri wa miaka 18 kutoka Palmeiras ya Brazil kwa   ada ya pauni milioni 25....
13/06/2024

imemsajili winga mashuhuri Guilherme mwenye umri wa miaka 18 kutoka Palmeiras ya Brazil kwa ada ya pauni milioni 25.5. Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitano.
Usajili huo ni wa kwanza kufanywa na kocha wao mpya Julen Lopetegui.
Usajili wake utakamilika kesho siku ya Ijumaa dirisha la usajili nchini Uingereza litakapofunguliwa.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255743975008

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Epl,La Liga,Serie A, Bundesliga-Kiswahili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share