04/11/2019
Haki ambazo zinaambatana na mali ya Marehemu
1. Kukafiniwa (kununua sanda), kuchimbiwa kaburi
na mambo ambayo yanahusika na maiti (katika
mazishi).
2. Kulipa deni adaiwalo.
3. Kutekeleza wasia ambao ameacha, na usizidi wasia
huo thuluthi moja ya mali.
4. Kugawanywa mali kwa wale wanaostahiki kurithi.
Sharti za kurithi
1. Kuwa na uhakika wa kifo cha mtu anae rithiwa, ima
kwa kushuhudia, au kwa kuhukumu kadhi, mfano: kwa
kupotea mtu muda mrefu sana.
2. Uhai wa wenye kurithi ima uwe wa uhakika au kwa
kukadiria, mfano: mama mwenye mimba.
3. Kujuwa ilimu ya mirathi, kuujua upande wote wa jamii
itakayo rithi.
Sababu za kurithi
1. Kwa uhusiano wa kizazi (Jamii)
2. Ndoa
3. Mtumwa aliye wachwa huru
Nguzo za kurithi
1. Anaerithiwa awe ameshafariki
2. Kupatikane wenye kurithi
3. Kuweko na kitu cha kurithiwa mfano: shamba, pesa n.k.
Mambo ambayo huzuiya mtu kurithi
1. Mtumwa harithi wala harithiwi, na iwapo amerithi basi
vyote alivyo vimiliki ni mali ya Bwana wake.
2. Muuwaji; mtu alieuwa kwa ajili ya kurithi, basi
hatopata kitu chochote katika mali ya yule anae mrithi,
kwa mujibu wa maneno ya Mtume Muhammad
(S.A.W)
" Hatopata muuaji mali ya katika mirathi ".
Imepokelewa na Muslim
Lakini kutokana na madhehebu manne yamekhitilafiana na
rai hii.
Hanafy:- Kila muuwaji atatoa kafara na atazuiliwa kurithi.
Malik:- Iwapo ameua kwa makusudi ndio harithi, la sivyo
basi atarithi.
Hanbal:- Kila muuwaji atadhaminiwa kwa dia;
Kisasi na kafara na hatorithi.
Shaffy:- Kuuwa kwa namna yoyote kutamfanya mtu
asirithi.
3. Kukhitilafiana kwa dini nayo ni: muislamu na asiye
kuwa muislamu hata k**a ni ndugu, haya ni kwa
mujibu wa maneno ya Mtume (S.A.W) " Hamrithi
muislamu kafiri wala kafiri hamrithi muislamu".
Imepokelewa na Bukhary na Muslim.
4. Mtoto aliezaliwa nje ya ndoa (isipokuwa ikiwa maiti
akiacha wasia).
Tofauti kati ya Mahruum na Mahjuub
Mahrum:- Ni mtu ambae amezuilika kurithi kulingana na
mambo yale matatu mf: mtumwa, muuwaji na utafauti wa
dini.
Mahjuub:- Kupatikana kwa mtu alie karibu zaidi na maiti
kuliko yule wa mbali mf: Babu harithi ikiwa baba wa
marehemu angali hai.
Daraja za wenye kustahiki kurithi
2. Aswabat nasabiya: hawa nikila ambae yuko karibu na
marehemu atachukuwa kilicho bakishwa na wenye furudh.
3. Aswabat sababiya: Naye ni mtumwa akiwa mume au
mke.
4. Aswabat m'utak: hawa ni jamaa wa mtumwa ikiwa
hayupo, basi hawa watarithi mahala pake.