01/05/2026
Kuna tukio la utapeli limetokea Bariadi mkoani Simiyu vijana waliojifanya wataalamu kutoka kampuni za simu wakiwa wamevalia Tisheti zenye majina ya makampuni hayo wamefika kwenye kibanda cha uwakala na kumkuta binti ambaye walimwambia wao ni wataalamu kutoka makampuni hayo na wanatembelea watoa huduma za miamala ili kuwaboreshea laini zao za uwakala
Wakamwambia binti awape namba ya simu ya boss wake waongee nae, wakampigia wakamuuliza tu kwa ufupi wewe ndio fulani mmiliki wa kibanda hiki cha uwakala alivyoongea kuwajibu wakaongea nae k**a salamu za kawaida kwa watoa huduma wakakata simu kisha wakamwambia binti tayari boss wako ameelewa maelekezo tuliyompa atapiga simu akupe maelekezo sasa hivi
Kumbe sauti ya boss wameshaikopi kwenye mfumo wa AI hatimaye wakapigiana kwa sauti ya boss wake na kumpa simu aongee nae binti huyo akawa anaskia sauti ya boss wake kabisa na kupokea maelekezo kwamba "Wape namba za siri hao jamaa na laini za miamala wafanye hayo marekebisho tu nshaongea nao ondoa wasiwasi"
Binti akawapa jamaa wameiba shilingi laki tano 😭😭😭😭😭🙌🙌🙌🙌
NB: Tukio hili limemkuta mtu wangu wa karibu kabisa, sio stori
Mnaofanya biashara ya uwakala chukueni tahadhari, matapeli wamekuja na mbinu mpya wanatumia AI