Itambue Thamani Yako -ity

Itambue Thamani Yako -ity MWANAMKE JIPENDE , JITUNZE , JIAMIN

Ity tunafanya kazi pia ya kutekeleza haki za watoto .Haya ni baadhi ya makundi ya Tasisi yetu yaliyoweza kutoa tabasamu ...
18/09/2025

Ity tunafanya kazi pia ya kutekeleza haki za watoto .
Haya ni baadhi ya makundi ya Tasisi yetu yaliyoweza kutoa tabasamu kwa watoto mbalimbali waliweza kula na kunywa na watoto na kuwapa mahitaji mbalimbali ya muhimu
Kupitia hili naomba nikumbushe :-

FAHAMU SHERIA ZA MSINGI ZA MTOTO
1. Mtoto ana haki ya kupewa jina na utaifa
Sheria ya Mtoto ya Sura ya 20 ya Mwaka 2009, kifungu cha 6 mtoto ana haki ya kuwa na utaifa, kupewa jina na kuwafahamu wazazi wake wa kibaiolojia.

2. kila mtoto ana haki ya kutoa maoni yao
Sheria ya Mtoto Sura ya 20 ya mwaka 2009, kifungu cha 11, mtoto ana haki ya kutoa maoni na maoni yake yapaswa kusikilizwa, kuheshimiwa na pia kupewa nafasi ya kushiriki kwenye kufanya maamuzi yatakayo pelekea ustawi wake.

3. Matunzo ya mtoto
Sheria ya Mtoto Sura ya 20 ya mwaka 2009, kifungu cha 17 inamtaka mtu yeyote anayemiliki sehemu ya starehe ikiwemo bar, au kilabu kutowaruhusu watoto kuingia maeneo hayo.
o Vile vile asiwauzie watoto sigara, pombe au kilevi cha aina yoyote. Na mtu atakaye kwenda kinyume na kifungu hicho tajwa atakuwa amefanya makosa na adhabu yake haitakuwa chini ya shilingi Milioni moja na isiyozidi milioni tano au kifungo jela kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na mbili.

4. Amri ya malezi ya Mahak**a iwe kwa faida ya mtoto
Sheria ya Mtoto Sura ya 20 ya mwaka 2009, kifungu cha 18 Mahak**a inaweza kuamua mtoto akae sehemu nyingine tofauti na wazazi wake k**a wazazi wake wapo hai ikiwa mahak**a itathibitisha kuwa usalama wa mtoto upo hatarini.

5. Amri ya matunzo na uasili wa mtoto
Sheria ya Mtoto Sura ya 20 ya mwaka 2009, kifungu cha 24, yakuwa ikiwa wazazi, walezi au ndugu wa mtoto ambaye yupo chini ya amri ya uangalizi hawaonyeshi kuwa na hali ya kujali maslai ya mtoto kwa namna yoyoyte kwa kipindi cha uangalizi kilichotolewa na mahak**a, mtoto anaweza kuasiliwa (adoption) na mlezi mweingine.

6. Haki ya mtoto pindi wazazi wanapotengana
Sheria ya ndoa ya Tanzania wazazi wakitengana kwa talaka mtoto ana haki ya;
-Kuendelea kupata elimu ya kiwango kilekile alichokuwa akikipata kabla ndoa ya wazazi wake haijavunjika.
-Kuishi na mzazi ambaye kwa maoni ya mahak**a ana uwezo wa kumtunza mtoto na uwezo wa kuzingatia maslahi bora ya motto.
-Na awe na uwezo wa kumtembelea mzazi mwingine wakati wowote atakapojisikia kufanya hivyo, ikiwa tu kufanya hivyo kutaingiliana na ratiba za shule au masomo.

Big shout out to my newest top fans! 💎Sarah AdamuDrop a comment to welcome them to our community,  fans
14/09/2025

Big shout out to my newest top fans! 💎

Sarah Adamu

Drop a comment to welcome them to our community, fans

Itambue Thamani yako Foundation Tanzania ni Taasisi inayojushughulisha na kupinga ukatili wa kijinsia kwa mama na mtoto ...
11/09/2025

Itambue Thamani yako Foundation Tanzania ni Taasisi inayojushughulisha na kupinga ukatili wa kijinsia kwa mama na mtoto hata baba anaepitia ukatili wa kijinsia,kusaidiana kwenye shida na Raha,kugusa jamii kwa kuwaona na kuwajali wafungwa,yatima wajane,wagonjwa watu wenye mahitaji maalum,wafungwa na wanaofanana na Hawa. Mpaka sasa Tasisi yetu ipo Kila mkoa na baadhi ya wilaya kwa asilimia kubwa.Kuwa karibu na page yetu ili uendelee kutufahamu na kutuelewa na kutuunga mkono pia.

TAASISI KUSHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFAViongozi ITY Taifa pamoja na wajumbe waliweza kuudhuria kongamano la NGO's  sisi k...
04/09/2025

TAASISI KUSHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA

Viongozi ITY Taifa pamoja na wajumbe waliweza kuudhuria kongamano la NGO's sisi k**a Taasisi ya Itambue Thamani Yako tuliwezakushiriki katika kongamano la kitaifa la NGO's lililofanyika katika ukumbi wa jakaya kikwete jijini Dodoma pongezi serikali na kwa kufanikisha kutuunganisha mashirika yoteyasiyo ya kiserikali na kutupa elimu mbalimbali tulijfunza mengi na huu umekua mwanzo mzuri kwetu k**a Taasisi.Tunashukuru kwa kupata vyeti vya ushiriki pia.

Pichani ,ni mwanamama Mtanzania iashie nje ya Tanzania kwa sasa , Mapenzi makubwa aliyo nayo mwana ITY mwenzetu huyu kwa...
16/05/2025

Pichani ,ni mwanamama Mtanzania iashie nje ya Tanzania kwa sasa , Mapenzi makubwa aliyo nayo mwana ITY mwenzetu huyu kwa ITY ni makubwa mno kiasi chakujikuta anachangia fungu kubwa ktk kikundi chake ili kuweza kufanikisha mipango ya kusaidia jamii ktk umoja wao.Ity hatuimbi upendo kwa maneno,bali tunatangaza upendo kwa matendo. ITY Kagera are lo lucky to have search a member .Wamama diaspora au wamama kutoka sehemu yoyote mnakaribishwa ktk umoja huu .Ni wajibu wetu kuisaidia jamii kwa kile kidogo MUNGU alichokujaalia ,kontakt uongozi ITY k**a utapenda kufanya charityyoyote ,iwe ktk kituo chocote cha watoto walioko ktk mazingira magumu.Kupitia ITY sadaka yako itawafikia walengwa bila utata wowote ule.Jongea.

Taasisi ya Itambue Thamani yako Tanzania kwa namna ya pekee kabisa tunapenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa sasa tunapati...
03/05/2025

Taasisi ya Itambue Thamani yako Tanzania kwa namna ya pekee kabisa tunapenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa sasa tunapatikana Tanzania nzima kila mkoa na wilaya nyingi sana kazi tunazo fanya zinaonekana, Dhumuni kubwa ni kuwakusanya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendea lengo Kubwa ikiwa ni kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kusaidiana kwenye shida na raha na kuwajali wenye uhitaji maaalumu. Napenda kutoa Shukrani za dhati kwa serikali yetu kwa ujumla kwa kutukubali na kushirikiana nasi katika Taasisi yetu,tumekua na viongozi wa serikali katika matukio yetu mbalimbali na wameweza kutushika mkono na kuona jitihada zetu Mungu awabariki sana kwa muda wenu kushiriki nasi na kutuunga mkono.
Katika picha hizi ni baadhi ya matukio yanayoendelea katika Taasisi yetu kikanda na kimkoa.Napenda kuwaalika wanaotamani kujiunga nasi katika umoja huu nafasi zipo kila mkoa mnakaribishwa sana.

02/05/2025
ITY Lake Zone yafanyika baraka tena baada ya kuandaa Event kubwa kwa mwaka huu, event ambayo iliyofanyika Mjini Kahama t...
17/10/2024

ITY Lake Zone yafanyika baraka tena baada ya kuandaa Event kubwa kwa mwaka huu, event ambayo iliyofanyika Mjini Kahama trh 5 october ikijumuisha baadhi ya mikoa kadhaa iliyopo ndani ya zone hyo.Mwenyekiti madam Frida Betty na viongozi wengine walishirikiana kwa pamoja na kutoa misaada ktk gereza la wanawake lilipo Mahali hapo , mgeni rasmi akiwa mbunge wa viti maalumu Shinyanga Mhe.Christine Mnzava.

Baada ya likizo fupi soon tunaibuka tena KTK harakati zetu za kusaidia jamii pamoja na kusaidiana sisi Kwa sisi .
11/07/2024

Baada ya likizo fupi soon tunaibuka tena KTK harakati zetu za kusaidia jamii pamoja na kusaidiana sisi Kwa sisi .

Hii si ya kukosa, tarehe imekaribia Tukutane Wote Rocky City Mall -Mwanza Kwa ajili ya Event yetu ya kukata na shoka för...
20/11/2023

Hii si ya kukosa, tarehe imekaribia
Tukutane Wote Rocky City Mall -Mwanza Kwa ajili ya Event yetu ya kukata na shoka för Morén information PLz call 0758484721 .

Address

Alhagsvagen 92
Dar Es Salaam

Telephone

+46737420237

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Itambue Thamani Yako -ity posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share