Mpehomediatz

Mpehomediatz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mpehomediatz, Photographer, P. O. BOX, Arusha.

31/05/2025

Mbuga ya Pili Serengeti

Viongozi Kazini kuwatumikia wananchi

NYUMBA  Ina  ,  ,     IPO WASSO Simu iitee. 0763-801111
13/08/2024

NYUMBA

Ina , ,

IPO WASSO

Simu iitee. 0763-801111

🏭NYUMBA INAUZWAIpo Sakala MAKALASINGAROOM 3  UMEME NA CHEMBA YA  MAJI TAKAKiwanja Ukubwa 20X20Simu iitee 0763801111
12/08/2024

🏭NYUMBA INAUZWA

Ipo Sakala MAKALASINGA
ROOM 3 UMEME NA CHEMBA YA MAJI TAKA

Kiwanja Ukubwa 20X20

Simu iitee 0763801111

09/08/2024

Kiwanja kinauzwa kitalu "E" mji wa Wasso huduma zote k**a maji na umeme zipo zinapatikan zinapatikan zinapatikan

05/08/2024
05/08/2024

KIWANJA KINAUZWA

KIPO WASSO

MTUMISHI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA  KUUZA DAWA Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Murtal...
03/07/2024

MTUMISHI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA KUUZA DAWA

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Murtallah Sadiki Mbillu amemsimaisha kazi Tabibu msaidizi Zahanati ya Misigiyo kupisha uchunguzi kwa tuhuma za Wizi wa dawa na vifaa tiba

Akizungumza ofisini kwake, Bwana Mbillu amesema kuwa amemsimamisha kazi Ndg. Samweli Panga ambaye ni Tabibu Msaidizi kwa kuk**atwa na dawa na vifaa vya vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi laki tatu na elfu 344 ,213.90 akiwa anaviuza katika soko la Olbalbal mnamo tarehe 13 Juni 2024.

Pia, Mkurugenzi amesema kuwa mtumishi huyo alikatwa baada ya kupata taarifa za siri na kuweka mtego ambao ulifanikisha kumk**ata akiwa na vifaa tiba na dawa ambavyo Serikali inatumia gharama kubwa vinunua.

Mkurugenzi ametoa onyo kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Ngorongoro kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma na hatosita kumchukulia hatua mtumishi atakayebainika kuwa na tabia wizi na kutojali kazi yake.

Aidha, Mganga mkuu wa Wilaya Daktari Libori Tarimo katika kuelezea suala hilo amesema amelaani kitendo hicho na hatomfumbia macho muhudumu yoyote wa afya atakayeenda kinyume na maadili ya kazi

"dawa za Serikali na vifaa tiba vitumike kwa lengo lilillokusudiwa na Serikali na sii vinginevyo" amesema Dkt. Libori.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya ngorongoro Bw.Murtalla Mbilu Ameanza utekekezaji wa maagizo ya Waziri Tamisemi Mh...
03/07/2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya ngorongoro Bw.Murtalla Mbilu Ameanza utekekezaji wa maagizo ya Waziri Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyoyatoa hivi karibu ya kuwajengea maafisa usafirishanji vituo(Bodaboda) kwaajili ya kuwawekea mazingira bora ya kufanyia kazi zao

Akizungumza na maafisa wasafirishaji hao(Bodaboda)katika Moja ya kituo Cha bodaboda wilayani hapo mkururugenzi huyo amesema utekelezaji huo umekuja baada ya waziri wa TAMISEMI kutoa maagizo kwa halmashauri zote nchini, kuwajengea maafisa usafirshaj vituo vya kuegesha vyombo vyao vya moto

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mohamed Bayo amewataka vijana hao kujiunga na Vikundi ili kunufaika na Mikopo ya Asilimia 4 ya Vijana inayotolewa na Halmashauri.

Aidha ameongeza kuwa maafisa usafirishaji hao wajiunge na vikundi na kutambuana ili kuweza kufahamiana na kutoa huduma bora kwa wananchi na kupunguza malalamiko ya wateja wanaopata madhara ya kuangushwa ama kuibiwa wakati wanatumia usafiri huo.

Afisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya ngorongoro bwana Daniel Bura amewasihi maafisa wasafirishaji hao kujiunga kwenye vikundi ili waweze kutambulika kwa sifa waweze kupata mikopo hiyo inayotelewa na Halmashauri

"Tunamshukuru Mhe.Raisi Samia suluhu hassan kwa kutemgeneza mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wakaazi wa Mamlaka ya mji mdogo wa wasso Loliondo ,hii imetuonesha jinsi gani serikali yetu inavyotujali,Amesema Bw.Lagwe Pemba

RC MAKONDA ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA MAJI WILAYANI NGORONGORO _Mradi huu unatokana na mahusiano mazuri ya Tanzania na Fa...
03/07/2024

RC MAKONDA ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA MAJI WILAYANI NGORONGORO

_Mradi huu unatokana na mahusiano mazuri ya Tanzania na Falme za kiarabu_

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Ndugu M***a Misaile na viongozi wengine wa serikali ya Mkoa na Wilaya ya Ngorongoro wametembelea na kukagua mradi mkubwa wa uchimbaji wa visima virefu vya maji vinavyochimbwa wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Mradi huo mkubwa wa maji unatekelezwa kwa pamoja na serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai inayoongozwa na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai ,bilionea na makamu wa Rais wa milki za kiarabu UAE ukiwa na malengo ya kuchimba visima virefu 37.

"Leo tunakuja kuwaambia kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwanadiplomasia namba moja, Mkuu wa nchi yetu na Rais wetu ametujengea mahusiano mazuri na nchi za Falme za kiarabu na sisi wana Ngorongoro tumeanza kuyaona matunda hayo ikiwa ni ndoto na shauku ya Makamu wa Rais Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.", amesema Mhe. Makonda.

Kulingana na taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, hadi sasa jumla ya visima 18 vimeshachimbwa kwenye vijiji mbalimbali, ambapo visima 12 kwenye vijiji vya Oloboo, Maaloni, Wasso na Siteti vimeshakamilika na wananchi wameanza kunufaika kikamilifu na mradi huo mkubwa wa maji.

Address

P. O. BOX
Arusha
1

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mpehomediatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category