Msafi the Comedian

Msafi the Comedian -Ke



10/04/2023

Leteni pages zunu tuwa follow mara hiyo
Meanwhile follow Msafi Davi Wa Imani

10/04/2023

Ndereva mwenye ujuzi halalamikii barabara yenye mitaro mikubwa .🤣🤣🤣🤣
Elewa swali

Send a message to learn more

11/03/2023

Chelsea ajeni kiburi, kupiga Leicester kwan n kuchukua kikombe

26/02/2023

Marseill GG
Psv win
Bayern m win
Barcelona win
United win
Take to the nearest bank

07/01/2023

Asifiwe mwokozi

27/12/2022

Morning 🌄 🌅 🌄 🌅 friends

26/12/2022

TUSALI SALA YA ASUBUHI.

+Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.

Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.

Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
______________________

Ee Baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi, nikutii.

Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.

Mlinzi mkuu malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.

NIA NJEMA.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.

Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.

Kwa utii navumilia
Teso na matata pia.

Nipe, Bwana, neema zako
Niongeze sifa yako. Amina.

•SALA YA MATOLEO.
Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie.

BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani k**a mbinguni.

Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, k**a tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.

SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi. Muumba wa Mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristo Mwanae wa pekee, Bwana wetu. Aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Akateswa kwa mamlaka ya Ponsiyo Pilato. Akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu. Siku ya tatu akafufuka katika wafu. Akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi. Toka huko atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo. Amina.

AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wengine.

2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.

3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.

4. Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.

AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria misa takatifu, dominika na sikukuu zilizoamriwa.

2. Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu.

3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.

4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa P***a.

5. Saidia kanisa katoliki kwa zaka.

6. Shika sheria katoliki za ndoa.

Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe malaika mlinzi wangu, nanyi watakatifu somo wangu, nanyi watakatifu wote, niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.

SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.

SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.

SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, k**a nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.

SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu nimetubu sana, niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe nwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako, nipate kurudi. Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.

MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

~Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyosema.

~Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

•Neno wa Mungu akautwaa mwili, akakaa kwetu.

~Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:
Tunakuomba Ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika, kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu; kwa mateso na msalaba wake, tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.

BIKIRA MARIA MALKIA WA AMANI, UTUOMBEE!

Tunawatakia siku njema kwa jina la +Baba na la +Mwana na la +Roho Mtakatifu. Amina.


14/12/2022

There are no limits to our dreams, just believe they do mean something to us.

02/12/2022

2hrs from Wednesday bado haijaisha kwan

14/11/2022

Ukihamia plot mpya kitu gani ya kwanza kuchunguza 🙉🙉🙉🙉🙉

30/09/2022

Matusi hutogea after break up huwa k**a gani

Address

Kitale

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msafi the Comedian posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category